HEADER AD

HEADER AD

ZAIDI YA WATU LAKI MBILI KUPATA VITAMBULISHO VYA NIDA KAGERA

Na Alodia Dominick, Bukoba

WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi Innocent Bashungwa amesema watu wapatao 269,177 mkoani Kagera wanatarajia kusajiliwa kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Nida.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo  Februari 28,2025 wakati akiwa mgeni rasmi kwa niamba ya makamu wa Rais Philip Insdor Mpango katika Jubilee ya miaka 25 ya utoaji huduma za Bukoba Kolping Hotel iliyopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Bashungwa amesema mkoa wa Kagera una watu zaidi ya milioni 3 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, watu milioni 1.3 wana miaka kuanzia 18 kwenda juu, miongoni mwa takwimu hiyo waliosajiliwa nida ni watu milioni 1.6 sawa na asilimia 80 ambao hawajasajiliwa ni 269,177 sawa na asilimia 20.

      Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Innocent Bashungwa akizungumza katika jubilee ya  miaka 25 ya utoaji huduma Bukoba Kolping hotel.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais  Samia Suluhu Hassan kutoa fungu la fedha mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuwasajili wananchi 269,177 ambao wameishatimiza miaka 18 na walikosa nafasi ya kujisajili  hapo awali ili upata vitambulisho vya Nida”

“Sasa hivi tuna fedha kwa ajili ya kusajili wananchi asilimia 20 ambao walikuwa bado, nimewaelekeza nida mkoa wa Kagera kuanza zoezi la usajili wa wananchi hao waliokuwa wamebaki na zoezi hilo litaanza Machi 10, mwaka huu na wataanzia wilaya ya Kyerwa wilaya nyingine zitafuata” amesema Bashungwa.

Ameeleza kuwa mkakati uliopo kwa sasa mwananchi baada ya kujisajili ndani ya siku saba atapokea namba yake ya nida na baada ya siku 14 atapata kitambulisho cha nida.

Waziri Bashungwa amewaelekeza viongozi wa Nida ngazi za wilaya na mikoa kupitia vyombo vya habari watoe ufafanuzi kwa wananchi ili waweze kufahamu utaratibu mpya wa utoaji huduma ambao unalenga kuondoa kero zote zilizokuwa zinalalamikiwa na wananchi kuhusu usajili wa kupata kitambulisho cha nida, uzalishaji wake na usambazaji wa vitambulisho hivyo.  

Ametoa rai kwa wananchi kuwa yanapofanyika mazoezi ya uhakiki au usajili katika maeneo yao wajitokeze kupata huduma ili kutatua changamoto zinazokuwa zinawakabili.

      Maadhimisho hayo yamehudhiriwa na watu mbalimbali wakiwemo watawa

Amesema Nida kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji wanaendelea na mazoezi ya uhakiki katika ofisi za usajili na kwamba kuna watu uraia wao una mashaka na wapo watu ni raia wa Tanzania wanastahili kupata vitambulisho vya Nida hivyo siyo sawa wanaostahili kupata vitambulisho kuendelea kuwekwa pamoja na watu wenye mashaka ya uraia.

“Idara ya wakimbizi ndani ya wizara ya mambo ya ndani watafanya zoezi maalum la kuangalia watu ambao wamekaa kwenye kapu hilo miaka mingi tuweze kuwaainisha wale ambao ni wakimbizi wapate Nida namba ya mkimbizi.

" Wale ambao ni walowezi tuwajue lakini ambao ni watanzania kwa mujibu wa katiba na sheria wapate vitambulisho vyao kwa sababu ni haki hili tunalisimamia” amesema Bashungwa

Kutokana na baadhi ya ofisi za Nida kuwa mbali na ofisi za uhamiaji amewaelekeza kukaa ofisi moja ili kuwahudumia wananchi kwa haraka kuliko mwananchi anatoka ofisi za nida anaenda uhamiaji kwani inasababisha wananchi kutumia muda mwingi katika kutafuta huduma.

Wakati huohuo Waziri Bashungwa akizungumzia jubilee ya miaka 25 ya huduma za Kolpin hotel ameupongeza uongozi wa hotel hiyo kwa uratibu na usimamizi mzuri wa uendeshaji wa hotel hiyo hadi hotel inafikia kuazimisha jubilee ya miaka 25.

Bashungwa aliuahidi uongozi wa Bukoba Kolping Hotel  kuwa serikali itaendelea kushirikiana na jimbo katoliki la Bukoba ili kuhakikisha changamoto zinazopaswa kwenda serikalini kufanyiwa kazi wanazichukua na kuzifanyia kazi.

Akisoma risara ya hotel hiyo meneja wa Bukoba Kolpin hotel Brother Aderik Pesha amesema kuwa, Bukoba Kolping hotel ni moja kati ya taasisi  inayomilikiwa na jumuiya ya Kolping Tanzania inasherehekea huduma jubilee ya miaka 25 ya huduma bora kwa wateja.

       Meneja wa Bukoba Kolping hotel Brother Aderik Pesha

Ameeleza kuwa, Bukoba Kolping hotel ilianza kutoa huduma mwaka 2000 ikijulikana kwa jina la Bukoba kilping house na ilikuwa hotel ya kwanza yenye ubora wa hali ya juu katika mkoa wa Kagera.

“Kutokana na mahitaji makubwa ya wateja Bukoba Kolpin ilijengwa upya ili kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malazi, ukumbi wa mikutano, na huduma za chakula” amesema Brother Pesha

Ametaja lengo la hotel hiyo kuwa ni kutoa huduma bora za malazi na ukumbi, kuimarisha utalii wa ndani na kutangaza utamaduni wa mkoa wa Kagera na hifadhi zake za asili kwa wageni wa ndani na kimataifa.

Brother Pesha amezitaja changamoto zinazokabili Bukoba Kolping hotel kuwa ni pamoja na ushindani kuongezeka kwa hotel nyingine kumefanya ushindani kuwa mkubwa na kuhitaji mikakati bora ya kuimarisha huduma maradufu.

Changamoto nyingine kodi za biashara ni kubwa ikilinganishwa na mapato hivyo kuathiri uwezo wa kuwekeza katika maboreho, kuna uhitaji wa kutosha ili kuimarisha ujenzi wa ukumbi mkubwa na vyumba vya kisasa ili kuboresha zaidi huduma.

Baba mlezi wa Kolping Tanzania Padre Ansigalius amesema wanapofanya tafakari kuhusu safari yao ya miaka 25 changamoto walizokumbana nazo na mafanikio waliyoyapata wanaunganika na Zaburi 34 aya ya tatu kwa kusema mtukuzeni bwana pamoja nami na tuliadhimeshe jina  lake pamoja.

Amewashukuru baraza la maaskofuTanzania kwa kuwalea na kutegemeza kwa hali na mali na kuwa uwepo wao katika jubilee hiyo ni upendo mkubwa na kuthamini nchango wa chombo hicho katika jamii pia alimshukuru mgeni rasmi.

No comments