HEADER AD

HEADER AD

TLS KAGERA YAHIMIZA JAMII KUFUATA TARATIBU SAHIHI KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO


Na Alodia Dominick, Bukoba

IKIWA imebaki siku moja kuhitimisha wiki ya sheria nchini jamii imetakiwa kufuata utaratibu sahihi ambao utaweza kusaidia migogoro kuisha na kuendelea kuishi kwa amani.

Rai hiyo imetolewa na makamu mwenyekiti wa chama cha mawakili Tanzania ,(TLS) mkoa wa Kagera wakili Seth Niyikiza wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya mada ya sheria za ndoa, ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya sheria nchini.


Anasema malengo ya ndoa ni kuishi kwa upendo, amani na kulea pamoja vile viumbe vilivyokuja duniani bila hiali yao, na kwa sababu vimeishaletwa visisurubiwe kwa sababu kuna tofauti baina ua wazazi wawili walioshirikiana kuvileta.

Niyikiza akizungumzia sheria ya ndoa anasema kuna wakati ambapo ridhaa ya mke na mume ya kuishi pamoja kutokana na mazingira mbalimbali inaonekana wazi watu hawa hawawezi kuendelea kuishi pamoja na msaada pekee uliopo ni kila mmoja kuishi mwenyewe na maisha yake kwa maana ya talaka.

"Sheria ya ndoa sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 imetoa mwongozo kwamba sasa pale ambapo upendo umekwisha watu hawa wapate msaada, kitu ambacho kitaangaliwa msaada pekee unaowezekana ni talaka au kutenganishwa".

"Hatua ya kwanza ambayo wahusika watafanya ni kwenda katika mamlaka ya bodi za usuruhishi ya ndoa ya kata" anasema Niyikiza 

Anaeleza kuwa wale ambao wako kwenye ndo kwa mujibu wa sheria ya ndoa bodi hiyo ya kata inawasikiliza ni kutokana na kifungu cha 101,102 na 103 vinaeleza uwepo wa bodi ya usuruhishi ya ndoa,  ambapo wale watu ambao wanahisi hawapatani tena kwenye ndoa au kuna mgogoro unaoweza kujeruhi ndoa hiyo na kuifanya isiweze kuendelea watasikilizwa na kusuruhishwa.

Vilevile kama itaonekana kwamba bodi hiyo imeshindwa kabisa kusuruhisha ndoa hiyo itatoa cheti kinachoonyesha kushindwa kusuruhishwa kwa ndoa hiyo na chetu hicho ndiyo hatua ya awali ya mashauri ya ndoa na baada ya kutolewa cheti hicho wahusika watakwenda mahakamani kwa ajili ya hatima ya ndoa hiyo.

Amezitaja mahakama zenye mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ndoa kuwa ni mahakama kuu, mahakama ya wilaya na mahakama ya Mwanzo.

"Katika kusikiliza mashauri hayo kuna vitu vya kutazama ambavyo ni je walikuwa katika ndoa kwa muda sahihi wa kuweza kuomba talaka ambao ni kuishi kwenye ndoa ndani ya miaka miwili, katika muda huo ambao wamekaa kuna kitu wamechuma pia watatazama je kuna watoto" anasema Niyikiza .

Hakimu mkazi mwandamizi katika mahakama ya wilaya Bukoba Flora Kaijage anasema kuwa, sheria ya ndoa imetaja kuwa mwanaume anayeona asiwe chini ya miaka 18 na mwanamke anayeolewa asiwe chini ya miaka 15 lakini kama kuna ulazima wa kwamba watu wafunge ndoa labda mtoto wa kike ana mimba wawe wamefikisha miaka 14 wote wawili.

"Lakini kibali inabidi kitolewe na mahakama kwa maombi kwamba kwa mazingira hawa watu hawajafikisha miaka ya kufunga ndoa lakini tunaomba kibari kwa sababu fulani, hao watu wanaweza kuruhusiwa, lakini kuna swala la hiari na umri na ili binti akubaliwe kufunga ndoa baba mzazi inabidi akubali, kama baba amefariki uhiari unatoka kwa mama/mlezi" anasema Flora.

" Kama itaonekana baba/mama/mlezi wanakataa kutoa kibali kwa sababu ambazo siyo za msingi sana mtu anaweza akapeleka maombi mahakamani na mahakama baada ya kusikiliza inaweza kutoa kibali cha mtoto ambaye hajafikisha miaka 18 kuweza kufunga ndoa.

Kaijake anataja ndoa ambazo ni batiri yaani haziruhusiwi kuwa ni pamoja na baba kumuoa mtoto wake, mtoto wa kumwasili, shanghazi, mjukuu, mjomba na  ndugu wengine wa damu.

Kwa upande wake kadhi wa mkoa wa Kagera Mubaraka Kalolola anasema ndoa kwa dini ya kiislamu ni ndoa ya ibada ili ihesabike kwamba ni ndoa lazima awepo anayoa na anayeolewa yaani mume na mke na kuwa uislamu hautambui ndoa ya jinsia moja.

"Dini ya kiisilamu hairuhusu dada wanaozaliwa pamoja kuolewa na mume mmoja kwamba mwanaume mmoja awaoe dada wawili wanaozaliwa pamoja hairuhusiwi" anasema kadhi Kalokola 

Aidha Mkaguzi msaidizi wa polisi dawati Bukoba  Betrida Minga anataja sababu za migogoro ya ndoa kuwa ni pamoja na changamoto ya kiuchumi, changamoto ya kidini, mabadiliko ya kitabia, hali ya ukatili ndani ya ndoa, utamaduni,mila na desturi na sababu za kiafya.

Ametaja madhara yatokanayo na migogoro kuwa ni pamoja na kutelekeza watoto, kuongezeka kwa magonjwa ya kuambukiza, kutokea vitendo vya jinai ambavyo ni mauaji na migogoro isiyoisha ndani ya familia.

Hata hivyo, kwa masirahi mapana ya mtoto mahakama inaweza kuamuru mtoto ambaye ana umri wa kulelewa na mzazi mmojawapo baba/mama asikae naye baada ya mahakama kuamuru wanandoa hao kuachana.



No comments