HEADER AD

HEADER AD

JELA MIAKA MITANO KWA WIZI WA NGURUWE

Na Samwel Mwanga, Maswa

WASHTAKIWA  wawili kila mmoja amefungwa miaka mitano jela kwa wizi wa nguruwe.

Waliokumbwa na adhabu hiyo katika mahakama ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ni Masunga Chenya(20)na Daud Elias(19)wakazi wa mtaa wa Sola mjini Maswa.

Kabla ya hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aziz Khamis kutoa hukumu hiyo leo jumanne Machi ,11,2025 , Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya Taifa ya mashtaka wilaya hiyo,mkaguzi msaidizi wa polisi,Vedastus Wajanga aliieleza mahakama kuwa kwa pamoja  waliiba nguruwe mmoja mwenye thamani ya Sh 500,000 mali ya Clerdes Donacian mkazi wa mtaa wa Sola wilayani humo.

Amesema kuwa tukio hilo lilitokea mwezi Septemba 2,2024 majira ya saa 11;00 alfajiri mara baada ya washitakiwa wote kuingia ndani ya  zizi la nguruwe linalomikiwa na Clerdes Donacian na kuiba nguruwe huyo ambaye ni dume na siku hiyo hiyo walikamatwa wakiwa naye katika mtaa huo wa Sola.

Taarifa zilifika kituo cha polisi wilaya hiyo na askari polisi wafika eneo la tukio nakukuta tayari washtakiwa wapo chini ulinzi wa wananchi wakiwa pamoja na kielelezo ambacho ni nguruwe.

Katika kesi hiyo Namba 31726/2024 walishtakiwa katika mahakama hiyo kwa makosa  mawili  la kwanza ni  wizi wa mifugo kinyume na kifungu cha 258 (1)(2) (a) na 268 (1)(3)cha  sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022 .

Na katika kosa la pili la kupatikana na mali idhaniwayo kuwa ni ya wizi kinyume na kifungu cha 312(1)(b) na( 2) Cha sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16  Kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Upande wa mashitaka ulileta jumla ya mashahidi watano na vielelezo viwili ambavyo vilitolewa mahakamani hapo ili kuthibitisha makosa waliyoyafanya washitakiwa.

Mara baada ya washtakiwa kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliiomba mahakama kuwapatia adhabu kali ili iwe funzo kwao na kwa jamii kwani matuko ya wizi wa mifugo yanaongezeka ndani ya wilaya hiyo na mkoa huo.




 Amesema kuwa washitakiwa ni vijana ambao wana nguvu za kuweza kufanya kazi  nakujipatia kipato halali na pia  vitendo hivyo vya wizi vinadidimiza kipacho cha mwenye mali na huweza kusabisha wananchi kujichukulia sheria mkoni na hatimae kusababisha mauaji. 


No comments