HEADER AD

HEADER AD

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI MWENGE WA UHURU

Na Gustaphu Haule, Pwani

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amefanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa utakaofanyika mkoani Pwani.

Uzinduzi huo utafanyika April , 2 ,2025 katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo Majaliwa ameeleza  kuridhishwa na kazi iliyofanyika na kamati ya maandalizi inayosimamiwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge huku akitoa maagizo ya  kufanya maboresho kwenye maeneo ya uwanja utakapofanyika uzinduzi huo.

Majaliwa amesema kuwa kamati ya maandalizi imefanya kila kitu kinachotakiwa katika uzinduzi huo na kwamba anaimani kupitia kamati hiyo itakamilisha vitu vidogo vilivyobaki na kufanya shughuli hiyo kuwa bora na yenye kufana.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali  Machi 30 wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.

Amesema uwanja wa shirika upo vizuri japo kuna changamoto ya baadhi ya maeneo ambayo yanatarajiwa kutumika na vijana wa Alaiki kuwa na mashimo yanayosimamisha maji ambapo ameigiza kamati hiyo kuona namna ya kufanyia maboresho.

"Sina mashaka na maandalizi haya na  nategemea uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu kuwa bora kuliko mwaka jana na hii imetokana na ushirikiano wa viongozi uliopo hapa ,"amesema Majaliwa 

Majaliwa amepongeza sekretarieti ya mkoa wa Pwani na Wilaya kwa maandalizi waliyoyafanya ambayo yamefanya kusimamisha baadhi ya shughuli zao na ametaka Mkuu wa Wilaya ya Kibaha na wakurugenzi kuendelea kusimamia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Mji Kibaha hili ni eneo lenu hivyo muendelee kujitoa kuhakikisha jambo hili linafanyika vizuri lakini naamini shughuli hii itakuwa bora kuliko maeneo mengine ambayo yalizindua mbio za Mwenge wa Uhuru,"amesema Majaliwa 

Amesema maboresho ya uwanja huo yaliyofanyika yameimarisha uwanja huo ambao hata mechi za ligi kuu zinaweza kufanyika hapo na kwamba Serikali itaona namna ya kuboresha zaidi ili hata michezo mikubwa ya mpira iweze kufanyika.

     Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wa kwanza kushoto akiambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ( katikati) kukagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa .

" Pia kwakuwa Tanzania tumepewa heshima ya kucheza mashindano ya CHAN ambayo yatafanyiika hapa mwezi wa nane na mahitaji ya viwanja ni mengi hivyo tutakuja kukagua hapa na CAF wakiridhika watatupa kibali kutumia kiwanja hiki," amesema

Majaliwa amewataka wananchi kutoka maeneo mbalimbali kujitokeza kushiriki uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kuungana na Viongozi wa Wilaya na kitaifa watakaohudhuria.

Sambamba na hilo lakini pia ameiagiza kamati ya maandalizi kuhakikisha inaongeza hamasa na kualika wananchi kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini huku akiyataja maeneo ya Ubungo,Mbezi na Wilaya zote za Mkoa wa Pwani .

Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi ,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema upande wa maandalizi wanaenda vizuri ikiwemo kukamilisha maeneo ya uwanja huo.

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi ,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyoifanya Mjini Kibaha .

Ridhiwani amesema kwenye miundombinu pia maboresho yamefanyika na vijana wa halaiki wameandaliwa vizuri na kwamba wako tayari kushiriki tukio hilo la uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Hata hivyo ,amesema wageni pamoja na wananchi 22,000 wanatarajiwa kushiriki uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa unatarajiwa kufanyika April 2 katika vwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.

No comments