AFUNGWA JELA MIAKA 30 KWA KUZINI NA KUMPA MIMBA MTOTO WAKE

Na Samwel Mwanga, Maswa
DAUD Mabele(38)mkazi wa kijiji cha Kakola kilichpo Kata ya Shishiyu wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, amehukumiwa kwenda jela miaka 30.
Pia ametakiwa kumlipa fidia ya Tsh. 200,000 mhanga baada ya kupatikana na hatia ya kuzini na binti yake wa kumzaa (jina limehifadhiwa) mwenye miaka 14 na kumpatia ujauzito.
Hukumu hiyo imetolewa Alhamisi, Aprili 24,2025 katika Mahakama ya wilaya ya Maswa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Aziz Khamis baada kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Kosa aliloshtakiwa nalo ni kuzini na maharimu(Mwanamme kujamiana na ndugu yake wa damu)kinyume na kifungu cha 158(1)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022
Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 6929/2025 upande wa mashtaka ulileta mashahidi watano akiwemo mhanga mwenyewe pamoja na kielelezo ili kuthibitisha mshtakiwa kutenda kosa hilo.
Mshtakiwa aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na ana familia inayo mtegemea.
Awali mahakamani hapo ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Maswa,Mkaguzi msaidizi wa polisi,Vedastus Wajanga kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika mwezi Septemba, 2024 majira ya usiku.
Amesema kuwa mshtakiwa huyo alifanya kitendo hicho nyumbani kwake baada ya mama wa mhanga ambaye ni mke wake kwenda nyumbani kujifungua.
Baada ya kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliomba mshtakiwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na onyo kwa wengine wenye nia au lengo la kufanya kitendo alichokifanya mshtakiwa.
Post a Comment