HEADER AD

HEADER AD

RC MARA AAHIDI KUWASHUGHULIKIA WANASIASA UCHWARA, WAPOTOSHAJI NA WACHOCHEZI



Na Dinna Maningo, Tarime

Mkuu wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amewataka wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu na kwamba hatowavumilia wanasiasa uchwara, wapotoshaji na wachochezi.

Ameyasema hayo hivi karibuni April, 14, 2025 Nyamongo,wilayani Tarime wakati akipokea madawati 310, viti na meza 295 vilivyotengenezwa kwa fedha za uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.

RC Evans amesema kwamba hatopepesa macho kwa mtu yeyote atakayeleta taflani yoyote mkoani Mara ikiwemo wilaya ya Tarime na kwamba taratibu zipo kisheria zifuatwe.

" Kuna watu wamekua wanapenda kufanya fujo, waambie kitakachowapata heee, nafasi hiyo haipo tuna nafasi ya utulivu tufanye maendeleo, sasa hivi tunasonga mbele , wanasiasa uchwara tutashughulika nao.

" Tutashughulika na wapotoshaji, wachochezi hawana nafasi katika mkoa wa Mara. Kuna wengine wamekuwa wakisubiri nyakati hizi za uchaguzi na kuanza kuzusha chokochoko, hazitakubalika na hazina nafasi .

" Kuna ambao walishazianzisha wamepata sindano yao, wale wengine ambao wanajipanga ili walete fujo na wao watapata sindano zao, sheria itafuata mkondo wake " amesema RC Mtambi.

No comments