DORKASI NYAMONGO SDA, NYANGOTO SDA, FAMILIA YA MCHUNGAJI EAGT WATOA MSAADA KWA WASIOONA TARIME
>>
Nguo, sabuni, fedha zatolewa
>> Afisa
Maendeleo Kata ya Matongo, Kemambo nao waguswa
>> TLB Tarime wawashukuru wadau
Na Mwandishi Wetu ,Tarime
MAANDIKO Matakatifu katika Biblia, kitabu cha Luka 3 fungu la 11 kinasema “ Akawajibu akiwaambia ,Mwenye kanzu mbili na ampe asiye ma kanzu; naye aliye na vyakula na afanye vivyo hivyo”.
Kitabu hicho
cha Luka 14 :13-14 kinasema “ Bali ufanyapo karamu waite maskini,vilema,
viwete, vipofu, nawe utakuwa heri ,kwakuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana
utalipwa katika ufufo wa wenye haki “.

Pia kitabu
cha Matendo 9 : 36 kinasema “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake
Tabitha , tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa
matendo mema na sadaka alizozitoa”.
Katika kutekeleza maandiko matakatifu ya Biblia , kikundi cha huduma ya wanawake (Dorkasi) katika kanisa la Waadventista Wasabato , Nyamongo Kati na Dorkasi katika kanisa la Nyangoto SDA wilayani Tarime ,mkoa wa Mara wametoa msaada wa fedha ,sabuni na nguo kwa wanachama wa chama cha wasioona (TLB) wilaya ya Tarime.
Kikundi cha Dorkasi Mei, 30, 2025 walifika katika ukumbi wa Ingwe sekondari -Nyamongo wakati wa mkutano wa wanachama wasioona waliokutana kwa ajili ya kujadili mambo ya chama kwa kipindi cha mwaka mzima.
Wasioona wakiwa kwenye mkutanoKatika mkutano huo walihudhulia pia wadau mbalimbali akiwemo afisa maendeleo ya jamii kata ya Matongo Neema Abel , afisa maendeleo ya jamii kata ya Kemambo Mary Kitesho Laizer, afisa ustawii wa jamii kata ya Matongo, Elias Masangora , Frola Eliud ambaye ni mke wa mchungaji Eliud Wilson wa kanisa la EAGT Nyamongo ,na kutoa msaada.
Mwenyekiti
wa Dorkasi Nyamongo Kati SDA , Sara Jonathani amesema Dorkasi ni kikundi
kilichopo ndani ya kanisa kinachosaidia watu wenye uhitaji na kinasaidia hata
walio nje ya kanisa la Waadventista Wasabato.
“Abia Orindo alitupatia mwaliko tukaona tuje tujumuike pamoja ,tumekuja na nguo, sabuni za unga zenye thamani ya Tsh. 60,000, pesa Tsh. 50,000 kwa ajili ya kutunisha mfuko wenu”amesema Sara.
“Kitabu cha Zaburi 34:18-19 kinasema Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,na waliopondeka roho,na waliopondeka roho huwaokoa. Fungu la 19 linasema mateso ya mwenye haki ni mengi,lakini bwana humponya nayo yote”.
Kikundi
hicho cha Dorkasi kikaimba wimbo wa kuwatia moyo wasioona wakisema kwamba, ni
wajibu wa kila mtu kusaidia ,nyoosha mkono wako kwa wahitaji utabarikiwa na
Mungu.
Mwakilishi
wa Dorkasi Nyangoto SDA , Ester Josephat Mwita, amewaomba wasioona kutokata
tamaa kwani Mungu anawapenda jinsi walivyo huku akiwasisistiza kufanya kazi na
kumwabudu Mungu na wakatoa Tsh. 50,000 kutunisha mfuko wa TLB na msaada wa nguo.
Flora Eliud mke wa mchungaji wa kaniasa la EAGT Nyamongo, Eliud Wilson amewatia moyo wasioona na kusema yupo pamoja nao huku yeye na familia yake wakichangia fedha na nguo na kuahidi kuendelea kusaidiana na kikundi hicho.
Msaada huo wa wanawake ukamgusa afisa maendeleo ya jamii kata ya Matongo, Neema Abel na kutoa Tsh. 50,000 kwa ajili ya TLB huku afisa Maendeleo Kata ya Kemambo ,Mery Laizer akiwagusa kwa Tsh. 30,000 na kuahidi ushirikianao na chama hicho.
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Matongo, Neema Abel akitoa fedha kwa ajili ya kusaidia Chama cha Wasioona wilaya ya TarimeAfisa Ustawi
wa Jamii Kata ya Matongo, Elias Masangora,amesema afisa ustawi wa Jamii ni
msimamizi mkuu kwa watu wenye ulemavu kwenye halmashauri na kwamba kata hiyo
haikuwa na afisa ustawi wa jamii hivyo ameahidi kushirikiana na chama hicho.
Mtunza hazina wa TLB Wilaya ya Tarime Bhoke Orindo amewashukuru Dorkasi Nyamongo , Dorkasi Nyangoto, familia ya mchungaji Eliud, mchungaji Alex Matiko, na wadau kutoka Nyamongo akiwemo Mkurugenzi kampuni ya WARACHA Daud Tindo ambaye ni mlezi wa kikundi hicho kwa kuwa bega kwa bega na kikundi hicho.
Mweka Hazina Chama cha Wasioona wilaya ya Tarime, Bhoke Orindo akizungumza, kulia ni Flora Eliudi.“Daud Tindo amekuwa akitusaidia sana kuhakikisha kikundi kinasonga mbele, Pia Mkurugenzi kampuni ya Rin, Isaack Range, KEMANYANKI, Gody Kubyo, John Jonathan, Maswa Sasi.
" Tunamshukuru Mama wawili , Werema Christopher aliyetuchangia Tsh. 800,000 na wengineo kufanikisha kikao hiki wamekuwa karibu na sisi kuhakikisha Chama kinasonga mbele .
"Tunamshukuru pia afisa maendeo ya jamii Kata ya Matongo, na wa kata ya Kemambo pamoja afisa ustawi wa jamii kata ya Matongo tunapowaalika wanafika na kutupa ushirikiano.
Ameongeza kusema "Tunamshukuru
mkuu wa wilaya ya Tarime Gowele ambaye
alikuwa ndio mkuu wa wilaya wa kwanza kufika kwenye kikao chetu cha wasioona na
kuendesha harambee iliyofanikisha zaidi ya Tsh. Milioni 8 kuchangwa huku yeye
akituchangia Tsh, Milioni moja, tunampenda sana tunomba siku nyingine atutembee
, lakini pia uongozi wa shule ya Sekondari Ingwe ambao umekuwa ukitupatia
ukumbi bure kufanya vikao vyetu “ amesema Bhoke.
Mwenyekiti
wa Chama cha wasioona wilaya ya Tarime Museti Mwita , amewashukuru wadau wote
ambao wamekuwa wakishirikiana na chama hicho ikiwemo kufanikisha vikao vya
chama, ukiwemo uwezeshaji wa gharama za usafiri, chakula pindi wanachama
wanapokutana kujadiliana masuala ya chama.
“Tunawashukuru
wadau wote mnaotuunga mkono hakika tunapata faraja sana tunapoona mnatushika
mkono. Tunamshukuru mwandishi wa Habari makini Dinna Maningo ambaye amekuwa
mstari wa mbele kuripoti Habari za watu wasioona.
“Mungu
akubariki sana kwa jitihada na akili zote unazotumia kwa ajili ya kuipaisha TLB,kupitia
wewe TLB Tarime imeweza kufahamika. Bila nguvu za waandishi wa
habaritusingefika hapa, maana wanaturusha na kazi zetu zinaonekana bila
waandishi wa Habari watu wasingejua yanayofanywa na TLB” amesema Mwenyekiti.
Chama cha
TLB kikamtunuku cheti cha shukrani mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mara , Nyamlanga
Rwakatare kwa ushirikiano Madhubuti na TLB wilaya ya Tarime.
Post a Comment