JESHI LA POLISI KAGERA LAPOKEA MAGARI SITA
Na Alodia Dominick, Bukoba
JESHI la Polisi mkoani Kagera , limepokea magari mapya sita aina ya Toyota land cruiser kutoka serikalini yatakayosaidia katika maswala ya ulinzi na usalama kwa wananchi mkoani humo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amepokea magari hayo ambayo hakutaja thamani yake mara moja na kuyakabidhi Mei 15, 2025 kwa wakuu wa polisi wa wilaya zilizopo mkoani Kagera ambazo ni Bukoba, Muleba, Missenyi, Karagwe, Kyerwa na Biharamlo huku gari la wilaya ya Ngara likiwa bado halijawasili.
Baadhi ya wakuu wa polisi wilaya za mkoa wa Kagera.Kamanda Chatanda amesema kuwa, lengo kubwa la kupewa magari hayo ni kuimarisha utendaji, kuhakikisha wanawafikia wananchi kwa wakati huko walipo.
"Naishukuru sana serikali ya Samia Suluhu Hassan mama katufanyia makubwa, kwa mara ya kwanza katika historia mkoa unapokea magari 14 kwa muda usiozidi miezi mitatu naomba niwahakikishie wananchi usalama kwao" amesema Kamanda Chatanda.
Amewatahadharisha watu wenye nia ovu kuwa Kagera haitakuwa sehemu salama kwao, kama wanadhani uharifu analipa wakaufanyie sehemu nyingine.

Wamewahakikishia wananchi kuwa, kupatikana kwa magari hayo ni uhakika mkubwa wa usalama wao na kuwa jeshi hilo linadaiwa na wananchi kwani wanahitaji kurudisha kile kinachohitajika kwani magari hayo yamenunuliwa kwa kodi zao.
Amewahakikishia ulinzi wa kutosha wananchi wanaotumia barabara kuwa zitakuwa salama, mapori yatapitika kwa usalama na hata tunapoelekea uchaguzi mkuu wananchi watapiga kura kwa amani.
Wakuu wa polisi wilaya
Post a Comment