HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI YAENDELEA KUSAFISHA ZIWA VICTORIA KUONDOA MAGUGU MAJI


Na Jovina Massano, Mwanza

SERIKALI inaendelea kuchukua hatua za makusudi kwa kusimamia sera ya mazingira ili kuendelea kulinda na kunusuru viumbe hai vyote, lengo likiwa ni kuhakikisha usalama wa viumbe hai unaimarika hapa nchini.

Katika ukanda wa ziwa Victoria eneo lililoathiriwa na Gugu maji la Busisi wilayani Sengerema na Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza , Mei, 15, 2025 zoezi la usafishaji wa ziwa unaendelea kufanyika ambapo Katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Cyprian Luhemeja amefika na kuona namna zoezi la usafishaji linavyoendelea.


Uondoshwaji huo unafanyika kwa kutumia mtambo wa kusafisha na kuchimba kina cha maji (Watermaster)wenye uwezo wa kusafisha ekali moja kwa siku ukiwemo ukataji kupitia vijana  wanaotumia  panga.

Aidha wakati zoezi hilo likiendelea tayari hatua zaidi zimeendelea kuchukuliwa ikiwa pamoja na ununuzi wa mitambo mitatu ambayo ipo katika hatua za awali.







          

No comments