HEADER AD

HEADER AD

KWANINI TEMBO WANACHUKIA NYUKI ?

 

gg

Chanzo cha picha,

Maelezo ya picha,Wakulima wanatumia nyuki kuwa wasaidizi katika kuwazuia tembo kwenye mazao yao.
  • Author,
  • N

WAKULIMA sasa wanawatumia nyuki kama njia mbadala na bunifu ya kuwalinda dhidi ya uharibifu wa tembo mashambani.

Katika maeneo mengi duniani, upanuzi wa mashamba umeanza kuingilia makazi ya tembo, hali inayosababisha migongano hatari kati ya binadamu na wanyama hawa.

Tembo wanapoingia mashambani, huharibu mazao na kutishia maisha ya watu.

Hata hivyo, nchini Kenya, baada ya miaka mingi ya utafiti, watafiti wamekuja na suluhisho rahisi lakini la ubunifu: uzio wa mizinga ya nyuki.

Mbinu hii imetokana na maarifa ya kutoka kwa mababu yaliyodumu kwa muda mrefu kwamba tembo hawapendi nyuki.

Kwa kutumia mizinga ya nyuki kama vizuizi, wakulima sasa wanaweza kuzuia tembo kwa njia isiyo ya vurugu.

Nyuki wanaotoa sauti kali wanapochokozwa huwatisha tembo, na kuwafanya waepuke maeneo ya kilimo.

Teknolojia hii rafiki kwa mazingira imeanza kutumika pia katika nchi nyingine kama Msumbiji na Thailand.

Lakini ni kwa nini tembo wanawachukia nyuki kiasi hicho?

Je, ni kweli nyuki wanaweza kuwa suluhisho la migogoro kati ya binadamu na wanyama pori katika dunia inayozidi kujaa watu?

"Hii ni mbinu ya asili, rahisi na yenye ufanisi ya kuwazuia tembo kuharibu mashamba. Inatumia kile ambacho tayari kinapatikana katika mazingira," anasema mtafiti Graeme Shannon.

Graeme Shannon, mtaalamu wa ikolojia ya wanyamapori kutoka Chuo Kikuu cha Bangor, Wales – Uingereza, ambaye amekuwa akichunguza tembo wa Afrika kwa zaidi ya miaka ishirini, anaeleza kuwa mara nyingi wanaohamishwa kuingia maeneo ya wanyamapori ni watu wa kipato cha chini.

"Kwao, kilimo ni uti wa mgongo wa maisha ya familia." Hata hivyo, maji safi na mazao yenye rutuba huwavutia tembo, na hivyo kuwakaribisha kwenye makazi ya binadamu.

"Wakulima hutumia muda mwingi na juhudi nyingi kulima mashamba yao, halafu tembo huja pale mazao yanapokaribia kuvunwa," asema Emmanuel Mwamba, mkulima kutoka kijiji cha Mwakoma, nchini Kenya eneo lililo katika mstari wa mbele wa migogoro kati ya binadamu na tembo.

"Tembo wakija… huondoka na kila kitu."

"Wengi wetu hutegemea mazao haya kwa chakula na maisha yetu ya kila siku," anaongeza Mwamba. "Fikiria mazao yote kuharibiwa usiku mmoja tu ni balaa."

Migongano kama hii inaweza kuwa na matokeo mabaya kwa pande zote.

Wakulima huweza kupoteza maisha wakijaribu kuzuia tembo wenye uzito wa tani saba wasiingie mashambani mwao, ilhali tembo nao hukumbana na hatari ya kuuawa kwa kuonekana kuvamia makazi ya binadamu.

Katika jitihada za kupunguza migogoro hii, wanasayansi na wanavijiji wamejaribu kwa miaka mingi mbinu mbalimbali za kuwazuia tembo kutoka uzio wa umeme, minara ya ulinzi, taa za sola, matofali yenye pilipili, hadi harufu kali za kuwakimbiza, au hata kelele kubwa kila moja ikiwa na mafanikio na changamoto zake.

Lakini mbinu moja imeibuka na kung'aa zaidi: kutumia nyuki kama walinzi wa mashamba.

Mbinu hii si tu huwazuia tembo kwa ufanisi, bali pia huwanufaisha wakulima kwa asali na mazao ya nyuki.

"Tulianza na uzio wa mizinga miwili tu. Sasa tuna zaidi ya mizinga 700 inayolinda vijiji vitatu," asema Mwamba kwa fahari. "Ni suluhisho lenye manufaa makubwa kwa jamii yetu."

Mwanzo wa wazo hili ulitokana na simulizi za jadi mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo Fritz Vollrath, mtaalamu wa ekolojia kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na mwenyekiti wa shirika la Save the Elephants, pamoja na Iain Douglas-Hamilton, mwanzilishi wa shirika hilo, walisikia hadithi kutoka kwa wafugaji wa Kenya kwamba tembo hujiepusha na miti yenye mizinga ya nyuki na hapo ndipo safari ya uvumbuzi ikaanza.

King alibuni njia ya kipekee ya kulinda mazao ya wakulima dhidi ya tembo kwa kutumia uzio wa mizinga ya nyuki.

Aliyajaribu wazo hili kwa mara ya kwanza mwaka 2008 katika kijiji cha Laikipia, Kenya, ambacho kilikumbwa mara kwa mara na uvamizi wa tembo.

Uzio huu una mizinga ya nyuki inayozunguka shamba, na mizinga hiyo imewekwa kila mita 10 kati ya nguzo mbili.

Nyuki wa asili wa Kiafrika huvutiwa kwenye mizinga kupitia harufu ya nta na mafuta ya mchaichai.

"Kwa ekari moja, unahitaji mizinga 24," asema King.

Hata hivyo, mizinga 12 kati ya 24 ni ya kweli, wakati mingine ni ya bandia mizinga ya mbao ya manjano inayozua madhihirisho ya kuwa kuna mizinga mingi.

kati ya nguzo mbili.

Hii hupunguza gharama na kuwapa nyuki nafasi zaidi.

"Tembo wanapokaribia, wanapata harufu ya nyuki na asali, na kuona masanduku ya manjano. Hawawezi kujua ni upi wa kweli, na ni upi wa bandia. Hii inakuwa hila inayofanya kazi," asema King.

Mbali na kulinda mazao, uzio wa mizinga hutoa faida nyingine kwa jamii zinazoutumia, kama vile kuleta kipato cha ziada kupitia uzalishaji wa asali.

"Kama mkulima ana asali na mazao, hiyo inatosha kuendeleza familia," asema Mwamba, ambaye sasa ni afisa wa mradi wa Save the Elephants, akifundisha wakulima wengine jinsi ya kujenga na kutunza uzio wa mizinga.

Pamoja na kuwazuia tembo, ua wa mizinga ya nyuki unaweza kuwasaidia wakulima kupata mapato ya ziada kwa kuuza asali.
Pamoja na kuwazuia tembo, ua wa mizinga ya nyuki unaweza kuwasaidia wakulima kupata mapato ya ziada kwa kuuza asali.

Wanawake "mara nyingi wanaathiriwa kwa njia isiyo sawa na migogoro ya tembo wa binadamu", anaongeza King.

''Mara nyingi ni wanawake ambao wanafanya kazi mashambani na wanahitaji kuwatisha tembo, na huhatarisha kujeruhiwa. Kwao, "kujisikia kuwa na uwezo zaidi katika hali zao kunamaanisha kwamba wanaweza kuendelea na kazi ya kutunza kaya zao, labda kurudi shuleni, labda kuhakikisha wanapata wakati wa kufanya mambo mengine," King anasema.

Kwa miaka mingi, King na watafiti wenzake wamekusanya ushahidi kuhusu ufanisi wa uzio wa mizinga ya nyuki nchini Kenya.

Leo hii, mbinu hiyo inajaribiwa na kuchunguzwa katika nchi nyingi, zikiwemo Tanzania, Msumbiji na Sri Lanka.

Ufanisi wake pia umethibitishwa nchini Thailand, ambako migogoro kati ya binadamu na tembo ni suala la kila siku.

Mwaka 2024, King na wenzake walichapisha utafiti wa muda mrefu uliochunguza ufanisi wa uzio wa mizinga ya nyuki kwa kipindi cha miaka tisa katika vijiji viwili vidogo vya kusini mwa Kenya: Mwambiti na Mwakoma, ambako anaishi Emmanuel Mwamba.

Jamii hizi hutegemea sana kilimo cha mazao kama kabichi na mahindi, ambayo huvutia tembo wengi wanaovuka kati ya upande wa Mashariki na Magharibi wa Hifadhi ya Taifa ya Tsavo, hifadhi yenye takriban tembo 15,000 ndio idadi kubwa zaidi ya tembo nchini Kenya.


Maelezo ya picha,Charity Mwangome akilima shamba lake kwa kutumia jembe karibu na uzio wa mzinga wa nyuki kuzunguka shamba lake katika Kaunti ya Taita Taveta, Kenya.

Watafiti walifanya kazi kwa ukaribu na wanavijiji, wakifunga na kukusanya data kuhusu uzio wa mizinga ya nyuki.

Katika utafiti huo, ilibainika kuwa kati ya tembo wapatao 4,000 waliokaribia mizinga hiyo, asilimia 75 walizuiliwa na uzio huo.

Aidha, wakulima walipata kiasi cha dola 2,250 (sawa na pauni 1,740) kutokana na mauzo ya asali.

"Nadhani huu ni ubunifu wa kipekee," anasema Shannon, ambaye hakuhusika katika utafiti. "Mna njia ya asili ya kuwazuia wanyama hawa kuvamia mashamba. Kwangu mimi, ni suluhisho la kuvutia."

Hata hivyo, Shannon anasisitiza kuwa utafiti huo pia umeonesha mapungufu ya mbinu hiyo.

Kwa mfano, wakati wa miaka ya ukame, idadi ya nyuki ilipungua kwa kasi kutokana na uhaba wa mimea inayotoa maua.

Mnamo mwaka 2018, mizinga ilikuwa bado inarejea hali ya kawaida baada ya ukame wa mwaka uliotangulia, na tembo wengi walivamia vijiji, ambapo uzio uliweza kuwazuia takriban asilimia 73 tu.

"Kama ilivyo kwa mbinu au kifaa chochote kimoja, kina changamoto na mipaka ya ufanisi wake," anabainisha Shannon.

Kwa upande wake, King anaeleza wasiwasi wake kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mizinga hiyo: "Iwapo ukame wa ghafla utaendelea kujirudia kila baada ya miaka minne badala ya kila baada ya miaka 15 hadi 20 kama ilivyokuwa zamani, basi hali itakuwa mbaya kwa sababu nyuki hawatapata muda wa kutosha kupona."

Anaongeza kuwa mvua nyingi pia huleta changamoto kwa nyuki, kwani huangusha maua kutoka miti na vichaka hali inayopunguza chanzo cha chakula cha nyuki.

Kwa mujibu wa watafiti, suluhisho linaweza kupatikana kwa kutumia mbinu mbadala sambamba na uzio wa mizinga ya nyuki, kama vile mkaa wa pilipili au minara ya uangalizi.

"Bila shaka, hakuna suluhisho moja linaloweza kutatua tatizo hili pekee," asema King.

Chanzo : BBC

No comments