MADUMU TUMEWATUA
MADUMU tumewatua, maji wanafurahia,
Vijiji yameenea, huduma twajivunia,
Hata mashuleni pia, maji wanayatumia,
Madumu tumewatua maji wanafurahia.
Hakuna tena kukesha, maji kuyasubiria,
Yaliyochimbwa yatosha, twamshukuru Jalia,
Mnyeke kasadikisha, kwa watu amejitoa,
Madumu tumewatua maji wanafurahia.
Ushindi kwa kina mama, kwa maji kuyatumia,
Imerejea heshima, na kwa mama zetu pia,
Wameipata neema, nyumbani wametulia,
Madumu tumewatua maji wanafurahia.
Pongezi twakupatia, kina mama vijijini,
Dua tunakuombea, akubariki Manani,
Salamu zetu pokea, jina lako twathamini,
Madumu tumewatua, maji wanafurahia.
Na salanka tutafika, maji kuwapelekea,
Tunawatoa mashaka, maji mtayatumia,
Uhakika yatafika, ombi nimelipokea,
Madumu tumewatua maji wanafurahia.
Mwishoni nimefikia, tufurahie huduma,
Maji tunajivunia, tena safi na salama,
Nguo zetu tunafua, yameshapita ya nyuma,
Madumu tumewatua maji wanafurahia.
Mtungi ni SirDody -Kilimanjaro Tanzania
0762396923 au 0675654955
Post a Comment