RC MARA ASEMA ILANI YA CCM IMETEKELEZWA , MIRADI MINGI YAJENGWA
Na Ada Ouko, Mara
MKUU wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ametoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 ambapo amebainisha miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali.
Akizungumza Mei, 22,205 katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM mkoani humo amesema taarifa hiyo ni ya kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba, 2024.
RC Evans amesema kwamba, Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) mkoa wa Mara wamefanikiwa kuongeza mtandao wa barabara za changarawe kutoka kilomita 1,399 mwaka 2020 hadi kilomita 2,425 mwaka 2025 sawa na ongezeko la asilimia 73.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 kwa kipindi cha Januari - Desemba 2024, Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Mara.
"Madaraja yaliongezeka kutoka madaraja 129 mwaka 2020 hadi kufikia madaraja 139 mwaka 2025, vile vile makalvati yameongezeka kutoka makalvati 2137 hadi makalvati 2613 sawa na ongezeko la asilimia 22.3" amesema Mtambi.
Rc Mtambi ameeleza kuwa sekta hiyo imepata mafanikio makubwa katika miundombinu ya afya, vifaa tiba, upatikanaji wa dawa pamoja na rasilimali watu.
Wajumbe wa CCM wakiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Mei, 22 mwaka , 2025 katika ukumbi wa ccm Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Amesema maboresho hayo yamewezesha upatikanaji wa huduma bora na nafuu kwa wananchi mkoani hapa na maeneo ya jirani, ambapo anabainisha kuwa miongoni mwa mafanikio hayo ni ujenzi wa Hospitali ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere naoendelea.
Mradi huo umefikia awamu ya tano na kwamba unatekelezwa na mkandarasi mkuu "Prince General Investiment LTD" kwa gharama ya Tsh. Bilioni 14.7.
Kulia ni Mbunge wa viti maalum( CCM) mkoa wa Mara, Ghati Chomete pamoja na Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara, wa pili kulia wakisoma Kablasha la Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2020 - 2025) Kwa kipindi cha Januari - Desemba 2024 katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara.
"Mkoa wa Mara una vituo 421 vya kutolea huduma za afya ambapo kuna Hospitali 21, za serikali ni 17, vituo vya afya 56, vya serikali ni 49, Zahanati 333 za Serikali ni 303 na Kliniki 11 zote za binafsi.
" Mkoa una upungufu wa vituo vya Afya 122 na Zahanati 147 na Nyumba za watumishi 286, mahitaji ni nyumba 421 hivyo upungufu ni nyumba 135" aliongeza Mtambi.
Miongoni mwa washiriki wa kikao hicho mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Mara, Rhobi Samuel amesema miradi ya maendeleo imetekelezwa vizuri kwa 95 asilimia huku akitaja miradi waliyoitembelea kuwa ni elimu, afya na maji.
" Pamoja na changamoto ya upungufu wa vituo vya afya 122 na zahanati 147, bado Serikali yetu ina mpango mzuri wa kuhakikisha kwamba vituo hivyo vya afya vinajengwa na vinatosheleza mahitaji ya wananchi kimatibabu.
" Sambamba na hilo pia katika mradi wa maji naomba nitoe wito kwa serikali kuongeza juhudi ili wananchi walio na ukosefu wa maji wanufaike na huduma hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara , Patrick Chandi akiwa kwenye kikao cha Halmashauri kuu kinachohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali wa Ilani ya CCM ya (2020 - 2025)
Post a Comment