HEADER AD

HEADER AD

MNYEKE NI MSHINDANI


MSHINDANI ni Mnyeke, hilo linafahamika,

Si mtu mwenye makeke, ametulia hakika,

Ni mazuri mabo yake, kwa kweli hana mashaka,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Kafanya mengi mazuri, jimboni wamkubali,

Si mtu mwenye kiburi, ni mwenye kuona mbali,

Mwanzo wake ni mzuri, Jimbo atalikabili,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Jimbo atalichukua, natamka hadharani,

Wapinzani watapoa, kamwe hawataamini,

Bure mtajisumbua, mkiweza jitoeni,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Jimbo tutakupatia, kwa kura tutaamua,

Sisi twakuhitajia, kura tutakupigia,_

Ni wewe unayefaa, Jimbo letu kuchukua,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Mengi umetufanyia, tumeyaona jamani,

Maji twayafurahia, kwa kuchota mabombani,

Furaha imezidia, watu wanakuthamini,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Ana upendo hakika, kwa watu wake jamani,

Mkono tutakushika, hatukuachi njiani,

Tumepata uhakika, akubariki Manani,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Umetengeneza njia, ya bungeni kufikia,

Umeamua kwa nia, tena umedhamiria,

Dua tutakuombea, akuinue Jalia,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Namaliza kuandika, heri ninakutakia,_

Tumepata kwa hakika, kiongozi mwenye nia,

Na kamwe hana mashaka, ni nzuri yake tabia,

Mnyeke ni mshindani Jimbo atalichukua.


Mtunzi ni SirDody - Kilimanjaro

No comments