RC MARA : PATO LA MKOA LIMEONGEZEKA
Na Ada Ouko, Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi amesema pato la mkoa huo limeongezeka kwa asilimia 28.3 kutoka Tsh. Trilioni 5.3 mwaka 2020 hadi Tsh. Trilioni 6.8 mwaka 2023.
Akitoa taarifa hivi karibuni ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 ,katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Desemba, 2024 aliyoiwasilisha Mei, 23, 2025 mjini Musoma, ameeleza mafanikio ikiwemo miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali.
Amesema mchango wa mkoa huo katika pato la taifa ni asilimia 3.6 na kwamba kipato cha mwananchi kimeongezeka kwa asilimia 25.7 kutoka Tsh. 2,210,591.72 mwaka 2020 hadi Tsh. 2,780,148.25 mwaka 2023.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Ilani ya chama cha mapinduzi(CCM) ya mwaka 2020 hadi 2025 kwa kipindi cha Januari - Desemba 2024, Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Mara.
" Kuongezeka kwa pato hilo la mkoa kumetokana na jitihada zinazofanyika katika kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo ni pamba, kahawa, mbogamboga, mifugo na uvuvi" amesema RC Mtambi.
Ameongeza kuwa mazingira mazuri yamewezesha sekta binafsi kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa hasa katika uchimbaji wa madini.
Amesema uanzishwaji wa masoko ya madini katika mkoa huo umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa pato ghafi sambamba na udhibiti wa utoroshaji wa madini.
RC Mtambi akizungumzia mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye uemavu asilimia 10 kwa mwaka 2024/2025 hadi Februari , 28, 2025, amesema kuwa, mamlaka za merikali za mitaa kwa mwaka 2024/2025 zimetenga asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Amesema mapato hiyo ni kwa ajili ya kuchangia mfuko wa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kutoka kwenye makusanyo ya vyanzo vya ndani halisia.
" Hadi kufikia mwezi Februari, 2025, Jumla ya Tsh. Bilioni 2.93 Zilikuwa zimekopeshwa kwa jumla ya vikundi 324(Wanawake 139, Vijana 99 na Watu wenye Ulemavu 86)" Amesa Mtambi.
Sekta za Uzalishaji
Amesema Serikali mkoani humo imeendelea kusimamia sekta ya kilimo ili kuhakikisha kinaendelea kuwa chenye tija na kinachotumia teknolojia ya kisasa.
Pia kuhakikisha Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) inaendelea kutekelezwa na kutoa mchango mkubwa katika usalama wa chakula, pato la Taifa, maendeleo ya sekta ya viwanda na huduma.
Ameongeza kuwa, katika kutekeleza hilo, Serikali imeimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo, kuimarisha huduma za ugani, kuimarisha huduma za umwagiliaji, kuwezesha upatikanaji wa masoko na kuhamasisha Sekta binafsi, vyama vya ushirika na kuanzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo.
Amesema miongoni mwa shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha sekta ya kilimo ili kuinua pato na tija ni kuweka mazingira wezeshi kwa wataalam wa ugani ili kufikisha huduma za ugani kwa wakulima ambapo jumla ya pikipiki 314, zimegawiwa kwa wataalam kwa lengo la kuwafikia wakulima wengi zaidi.
Sambamba na hilo kuhamasisha wakulima wadogo 236,449 na kutengeneza mfumo imara wa kilimo ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kilimo cha kisasa, masoko ya uhakika na bei nzuri ya mazao.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Patrick Chandi akiwa kwenye kikao cha Halmashauri kuu kinachohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali wa Ilani ya CCM ya (2020 - 2025)
Post a Comment