HEADER AD

HEADER AD

BARRICK NORTH MARA YAHIMIZA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI


Na Dinna Maningo, Tarime 

UKATAJI Miti kwenye kingo za mto una madhara mengi kwa mazingira , maisha ya watu na viumbe hai.

Madhara hayo ni pamoja na kusababisha udongo kubomoka na kusombwa na maji, jambo linaloleta mabadiliko kwenye mkondo wa mto, kupungua kwa ubora wa maji, kupungua kwa viwango vya maji, kupotea kwa makazi ya viumbe hai.

Pia ukataji wa miti ni hatari kwa jamii za binadamu kwani kunawezesha kuongeza uwezekano wa mafuriko , mafuriko kuharibu makazi , mazao, miundombinu .

Katika kuhakikisha mto Tighite haukumbwi na madhara ya mmomonyoko wa udongo, Mgodi wa dhahabu Barrick North Mara, uliopo Nyamongo, wilayani Tarime, mkoani Mara, umeadhimisha siku ya mazingira Duniani kwa kupanda miti wakishirikiana na viongozi wa serikali za vijiji vinavyozunguka mgodi.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambikoamesema kuwa Dhamira ya mgodi ni kupanda miti ya asili 50,000  katika kingo za mto Tighite ili kuzuia mmomonyoko wa udongo kwa kushikilia udongo kwa mizizi yake ikiwemo na miti ya mbao itakayopandwa mita 60 za mto huo.

       Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko akipanda mti

Amewahimiza wananchi katika vijiji 13 vinavyozunguka mto Tighite wahakikishe wanatunza vyema miti hiyo kwani miti inayopandwa kwenye kingo za mto inazuia mmomonyoko wa udongo kwenye kingo za mto.

"  Hii Programu inahusisha upandaji wa miti takribani 50,000 ,tumeanza sasa hivi. Ni katika kuadhimisha siku ya mazingira Duniani. Tumeona ni muhimu sana na programu hii itaendelea katika maeneo 5 ambayo yapo pembezoni mwa mto Tighite.

" Programu kama hizi ziliwahi kufanyika mto Mara . Dhumuni letu ndani ya mwaka mmoja tuwe tumekamilisha Programu hii ya upandaji miti 50,000 " amesema Meneja.

" Tunapanda miti hadi mita 60 itakayotumika kunufaisha vijiji katika shughuli za kiuchumi " amesema Meneja.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji wa maji mto Tighite chini, Mwita Seri amesema kazi yake ni kuwasaidia bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria kuhakikisha wananchi wanatunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

     Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji wa maji mto Tighite chini, Mwita Seri akipanda mti.

" Nimepokea kwa mikono miwili hili zoezi la upandaji wa miti maana hatuwezi kuishi na vyanzo vya maji vilivyoharibuka havina mtu wowote, miti imekatwa sasa tunarejesha uoto wa asili" amesema Mwita.

Mkazi wa Kijiji cha Musege , Sara Lucus ameushukuru mgodi na kuomba zoezi hilo la upandaji miti liwe endelevu .

Pia amewasisitiza wananchi kutokata ovyo miti kwani ndio inachangia kuleta mvua .

         Mkazi wa Kijiji cha Musege , Sara Lucus akizungumza 

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Matongo, Charles Ryoba, ameushukuru Mgodi kwa kuadhimisha siku ya mazingira Duniani, kwa kupanda miti katika Kijiji chake na kwamba hatua hiyo inaweza kushawishi wananchi wanaopakana na mto nao kuweza kupanda miti katika makazi yao.

     Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Matongo, Charles Ryoba( katikati) upande wa mbele, akizungumza.

" Miti hii iliyopandwa itasaidia kutunza mto lakini pia inaweza kuwa ni shule watu wengine kujifunza . Watu wengine wana maeneo karibu na mto lakini wanauharibu kwa shughuli nyingine .

" Tukipanda kwa namna hii, ni shule ambayo watu watajifunza , na itanufaisha Kijiji kwakuwa kati ya miti itakayopandwa mingine ni ya mbao ambayo itainua uchumi wa Kijiji .

Kila tarehe 5, Juni ya kila mwaka ,Watanzania huungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliamliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972.

Lengo la maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ni kuhakikisha jamii Duniani kote kuelewa masuala yahusuyo mazingira na pia kuhakikisha Dunia  inakuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda Mazingira.


Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu wa 2025 ni ' Tumia mifuko mbadala wa prastiki; kwa ustawi wa Afya , mazingira na maendeleo ya uchumi

Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma,tarehe 5, Juni, 2025. Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Philip Mpango.
Meneja mahusiano mgodi wa Barrick North Mara, Francis Uhadi akizungumza ( kulia aliyevaa miwani)










Viongozi wa serikali za vijiji vinavyozunguka Mgodi wakiwa kwenye zoezi la upandaji miti pembezoni mwa mto Tighite, Nyamongo wilaya ya Tarime.


       Mfanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara, akipanda mti kati siku ya maadhimisho ya utunzaji wa mazingira 









Mto Tighite 











No comments