WATU WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA UBAKAJI KYERWA
Na Alodia Dominick , Kyerwa
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha baada ya kupatikana na makosa ya ubakaji wa watoto wawili kwa nyakati tofauti.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwakwe jana , Mwanasheria wa Serikali Dickson Makoro amesema adhabu hiyo kali ilitolewa baada ya washitakiwa kupatikana na hatia kutokana na mahakama hiyo kulidhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa Jamhuri pasipokuacha shaka lolote.
Dickson amemtaja mtuhumiwa wa kwanza kuwa ni Festo Mbeu mwalimu wa awali (42) mkazi wa kijiji cha Kaitambuzi alimbaka mtoto wa umri wa miaka nane.
" Tukio hilo lilitokea Julai , 22 mwaka 2024 ambapo Festo alimuamuru mtoto huyo baada ya masomo abaki shuleni kisha akampeleka kwenye moja ya darasa na kutandika mkeka akimtaka mhanga alale lakini alikataa"
Amesema baada ya mtoto huyo kukataa mshitakiwa alimlazimisha kumvua nguo za ndani na kumbaka kisha akamtishia kuwa asimwambie mtu yoyote, lakini mtoto huyo alipofika nyumbani alimueleza mama yake kuhusu kitendo hicho alichofanyiwa na mama alimkagua na kukuta shahawa sehemu ya ukeni.
"Baada ya mama huyo kuona hari hiyo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji kisha kutoa taarifa polisi, upande wa Jamhuri walikuwa na mashahidi watano akiwemo mhanga mwenyewe.
Kutokana na kanuni ya adhabu kifungu cha sheria 131(3) na 130 (1)(2) (e) cha kosa ambavyo ameshitakiwa navyo ametiwa hatiani na kufungwa kifungo cha maisha" amesema Mwanasheria.
Katika tukio la pili Mwanasheria huyo amemtaja Vicent Warundu mwenye miaka 24 , mkazi wa kijiji cha Muhulile Wilaya ni Kyerwa ambapo alihukumiwa kufungwa maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye miaka tisa.
Amesema mnamo mwezi, Agosti mwaka jana mshitakiwa Vincent alifika nyumbani kwao mhanga majira ya saa mbili za usiku kama alivyokuwa akifanya siku zote kwasababu ni jirani yao ambapo alimkuta mtoto huyo nje akiota moto wakati mama yake alienda dukani.
"Mhanga alienda nyuma ya nyumba yao kukojoa ambapo mshitakiwa aliaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani ndipo alimfuata mtoto huyo na kumziba mdomo na kumpeleka kwenye migomba na kumbaka na kumtaka asiseme kwa mtu ambapo mama yake aliporudi aliamua kumueleza" amesema.
Amesema baada ya mama huyo kuelezwa aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi Nkwenda na kufanikiwa kumkamata mshitakiwa Vicent.
Kesi hizo mbili zilisikilizwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya Wilaya Kyerwa Alen Ifunya ambapo aliwatia hatiani kwa mujibu wa kifungu vya Sheria kanuni ya adhabu kifungu cha sheria 131(3) na 130 (1)(2) (e)
cha kosa kufungwa ambapo pia alimhukumu Vicent kufungwa maisha.
Post a Comment