CCM NI IMARA
NAANZAJE kukihama, Chama bora Tanzania
Ni yake kubwa heshima, vijana imewalea
Imara kimesimama, nchi kimezikomboa
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Viongozi kimetoa, bora na wenye thamani
Hiki chama chavutia, hakika ni kishindani
Amani chasimamia, wanachama hongereni
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Ni mbali kimetutoa, na bado kipo imara
Chama tunajivunia, hakika ni chama bora
Mengi kimetufanyia, udumu wake ubora
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Udini kinalaani, kinahubiri amani
Chajulikana nchini, sisiemu ni makini
Watu kinawathamini, ni nzuri yake ilani
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Rais wake makini, ni mwanamke jasiri
Kwa kweli ni mshindani, kwa kuongoza hodari
Nchi ameithamini, Samia ni jemedari
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Mwishoni naelekea, shairi ninalitua
Ni nani wakuitoa, sisiemu imekua
Sifa zake meenea, sote tunajivunia
Si leo tangu zamani sisiemu ni imara
Mtunzi ni SirDody Kilimanjaro
(_Mudio Seminary Islamic high school_) 0675654955 au 0762396923
Post a Comment