MITANO NENDA KAMALIZIE RAIS SAMIA SULUHU HASSANI
ANATUTOSHA Samia, mitano twakupatia,
Ikulu utasogea, mitano kumalizia,
Kura tutakupigia, uchaguzi twangojea
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Uchumi umeinua, matunda , twafurahia,
Biashara zimekua, chakula twajipatia,
Kitini umetulia, hakuna wakukutoa,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ajira umezitoa, kwa watumishi wa umma,
Pongezi twakupatia, imara umesimama,
Umeme umeenea, gizani umetutoa,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Viwanda metujengea, uchumi wazidi kua,
Kipato twajipatia, familia twazilea,
Viwanda twategemea, kazi vinatupatia,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Treni ya mwendokasi, safari merahisisha,
Tushukuru kwa kiasi, nchi umeing'arisha,
Tunayaona mepesi, uhakika wa maisha,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ajira amezitoa, kwa kada ya ualimu,
Pongezi twakupatia, maisha yako yadumu,
Mengi ametufanyia, kuyakumbuka muhimu,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie
Huyo ndiyo jemedari, rais mama Samia,
Ni mwanamke jasiri, apewe yake maua,
Kwa kuongoza hodari, rais mama Samia,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ni rais mshindani, kimataifa na ndani,
Kaushika usukani, amri jeshi jamani,
Hata kule marekani, mama wanamthamini,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Mitano twakupatia, kwenda kuimalizia,
Heri tunakutakia, mpendwa mama Samia,
Mwishoni nimefikia, mengi nimeelezea,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie
MITANO NENDA KAMALIZIE RAIS SAMIA SULUHU HASSANI
ANATUTOSHA Samia, mitano twakupatia,
Ikulu utasogea, mitano kumalizia,
Kura tutakupigia, uchaguzi twangojea
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Uchumi umeinua, matunda , twafurahia,
Biashara zimekua, chakula twajipatia,
Kitini umetulia, hakuna wakukutoa,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ajira umezitoa, kwa watumishi wa umma,
Pongezi twakupatia, imara umesimama,
Umeme umeenea, gizani umetutoa,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Viwanda metujengea, uchumi wazidi kua,
Kipato twajipatia, familia twazilea,
Viwanda twategemea, kazi vinatupatia,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Treni ya mwendokasi, safari merahisisha,
Tushukuru kwa kiasi, nchi umeing'arisha,
Tunayaona mepesi, uhakika wa maisha,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ajira amezitoa, kwa kada ya ualimu,
Pongezi twakupatia, maisha yako yadumu,
Mengi ametufanyia, kuyakumbuka muhimu,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie
Huyo ndiyo jemedari, rais mama Samia,
Ni mwanamke jasiri, apewe yake maua,
Kwa kuongoza hodari, rais mama Samia,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Ni rais mshindani, kimataifa na ndani,
Kaushika usukani, amri jeshi jamani,
Hata kule marekani, mama wanamthamini,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie.
Mitano twakupatia, kwenda kuimalizia,
Heri tunakutakia, mpendwa mama Samia,
Mwishoni nimefikia, mengi nimeelezea,
Twende pamoja Samia mitano kamalizie
SirDody Dody, Kilimanjaro_(*Mudio Islamic seminary high school)*
0762396923.
Post a Comment