HEADER AD

HEADER AD

MADAKTARI BINGWA 64 WATUA PWANI KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI


Na Gustaphu Haule, Pwani
 
TIMU ya madaktari bingwa 64 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan imepokelewa leo Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza kazi maalum ya  kutoa huduma ya matibabu na uchunguzi wa wananchi wa maeneo mbalimbali yaliyopo mkoani Pwani.

Timu hiyo imepokelewa Juni 9, 2025 katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani na Mganga mkuu wa mkoa huo Kusirye Ukio akiwa amemwakilisha katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Rashid Mchatta.

Akizungumza katika hafla ya kuwapokea madaktari hao Ukio amewapongeza madaktari hao kwa utayari wao huku akiwaomba kwenda kujitoa kwa ajili kuwasaidia wananchi na jamii kiujumla katika kupata huduma bora ya uchunguzi na matibabu.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani (RMO) Kusirye Ukio akizungumza na madaktari bingwa wa mama Samia walipowasili leo Juni 9,2025.

Amesema kuwa Rais Dkt.Samia ameanzisha jambo kubwa na nzuri lenye maslahi ya wananchi wake na kwamba anataka kuona kampeni hiyo inakuwa na msaada Kwa Watanzania wote katika kuwaondolea changamoto za kimatibabu zinazowakabili.

Amesema katika kufikia malengo ya Rais Samia madaktari ndio wamepewa heshima na dhamana kubwa ya kufanyakazi hiyo huku akisema ni vyema sasa wakafanyekazi bila kuchoka na wakajitume kwa nguvu na uwezo wao wote.

Amewatoa wasiwasi madaktari hao kuwa maeneo waliyopangiwa yapo vizuri kwakuwa miundombinu imeboreshwa na kuwekwa vifaa vya kutosha vitakavyorahisisha utendaji wa kazi zao.

        Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kusirye Ukio (katikati)akiwa na baadhi ya madaktari bingwa wa mama Samia leo Juni 9,2025


"Najua mpo madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali na wauguzi kwahiyo niwaombe msichoke ,nendeni mkawahudumie wananchi na mkawape huduma sahihi lakini  mkatangaze upendo na msiogope kusema ukweli ,"amesema Dr Ukio.

Pamoja na mambo mengine,Ukio amewaomba madaktari hao katika kutoa huduma wahakikishe wanawasimamia vizuri wataalam wengine ili kuhakikisha huduma inayotolewa inakuwa bora zaidi.

Ameongeza kwamba mkoa utayafanyia kazi yale yote yatakayojitokeza katika zoezi hilo kwakuwa lengo la Rais Samia ni kutaka kuboresha huduma ya afya hapa nchini.

Naye afisa programu kutoka Wizara ya afya Joachim Masunga ,amesema kuwa madaktari hao wanatoka katika hospitali mbalimbali hapa nchini ikiwemo hospitali ya Taifa Muhimbili.

       Afisa programu kutoka Wizara ya afya Joachim Masunga akizungumza na madaktari bingwa wa mama Samia walipowasili Juni 9,2025 Mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema kuwa,timu hiyo itafanyakazi kwa muda wa siku tano na mgonjwa atapata huduma ya kibingwa papo hapo na wale ambao watagundulika kuwa na shida zaidi utaratibu mwingine utafanyika.

Ametaja baadhi ya magonjwa yatakayochunguzwa kuwa ni magonjwa ya Wanawake na Uzazi, magonjwa ya watoto,Upasuaji , dawa za usingizi, magonjwa ya ndani na magonjwa ya kinywa na meno.

Mratibu wa timu ya madaktari bingwa mkoa Pwani , Aden Mpangile,amesema mpaka sasa zoezi linaendelea vizuri kwa kila Halmashauri ambapo amewaomba Wananchi kujitokeza na kutumia fursa hiyo Kwa ajili ya kuchunguza afya zao.

      Mratibu wa timu ya madaktari bingwa wa mama Samia Dr.Aden Mpangile katika kikao cha madaktari hao kilichofanyika Juni 9,2025 katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Pwani.

Daktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Uzazi Dr.Mdoe Gumbo kutoka katika Manispaa ya Kibaha  amesema yeye na wenzake wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kikamilifu kwa jamii .

        Madaktari bingwa wa Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan wakiwa katika kikao cha pamoja na mganga Mkuu wa mkoa mara baada ya kupokelewa Leo Juni 9,2025.


No comments