HEADER AD

HEADER AD

MASHA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA


Na Nashon Kennedy , Mwanza

MBUNGE wa Zamani wa Jimbo la Nyamagana Lawrence Kego Masha, amejitokeza na kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Akizungumza na DIMA Online, Juni, 30,2025, amesema ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa uwezo wa kuongoza anao na kwamba jimbo la Nyamagana ni nyumbani kwao.

Amesema wakati akiwa mbunge wa jimbo hilo la Nyamagana alifanya mambo makubwa ya kimaendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu na shughuli nyingine za kiuchumi.

Aidha amesema yeye kama kijana bado ana uwezo mkubwa wa kuongoza na yuko tayari kuwatumikia wakazi wa Nyamagana

" Nina uwezo na dhamira ya kuendelea kuwatumikia wana nyamagana ili niweze kutimiza na kutekeleza mambo ya kimaendeleo na ni tumaini wana Nyamagana wataniunga mkono, amesema Masha.

Masha amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana mwaka 2005- 2010 na kushika nyadhifa mbalimbali  serikalini.

Amewahi kuwa Naibu na Waziri wa Mambo ya Ndani ( 2006-2008, Waziri wa mambo ya ndani , ( 2008-2009) , Naibu Waziri wa Nishati na Madini ( 2006-2006.

Masha ni miongoni mwa watiania waliopandisha joto la  kisiasa katika jimbo la Nyamagana kwa kujitokeza kuwania ubunge kwa mara nyingine  katika jimbo hilo mkoani Mwanza.




No comments