HEADER AD

HEADER AD

MKOTYA SHUJAA WA MAENDELEO CHEMBA


TUNAE mtu makini, mwenye dhamira na nia,

Ni mwanachemba jamani, ubunge kadhamiria,

Ni mjuzi mwenye fani, jimboni anatufaa,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


Kwenye kura za maoni, jina lake litapita,

Nayasema si utani, tena bila ya utata,

Litarudishwa jimboni, jina la ndugu Mkotya,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


Najua wanachukia, wanatamani kulia,

Wenye chuki nawajua, ni kweli wanaumia,

Hawataki kusikia, ubunge unawania,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


Wanasema vipembeni, eti umefanya nini?

Wakwao kafanya nini, mkiweza tujibuni,

Ni pesa wanathamini, wamejitoa nyumbani,

 Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


Kula wanapambania, wasije baki na njaa,

Wewe wanakuchafua, kwa pesa kujipatia,

Ugeni wanasifia, riziki kujipatia,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


Kaeni kwa kutulia, ujumbe nawapatia,

Mkotya twawaletea, ni jasiri mwenye nia,

Nyie kuleni rupia, jazeni matumbo pia,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


 Namaliza kuandika, shairi ninalitoa,

Mengi nimeyaandika, mazuri yakuvutia,

Oktoba uhakika, ushindi kujipatia,

Oktoba tunatiki kwa ndugu yetu Mkotya.


SirDody(Mudio Islamic seminary) ,0675654955 ,0762396923.

Karibu tukutungie shairi kupitia DIMA Online , mashairi ya kiuchumi, siasa, uwekezaji n.k

No comments