MKOTYA WA MRIJO SHUJAA ANAYETARAJIA KUUNGURUMA BUNGENI
NI mtetezi hakika, mengi atatupatia,
Kwa kweli hana mashaka, kura tutampatia,
Oktoba ikifika, kura utajipatia,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Jimbo analifahamu, si mgeni sikieni,
Yale yote ya muhimu, kwetu atayathamini,
Kijana mwenye nidhamu, Mwenyezi katuletea,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Tukatiki oktoba, kwa kijana wa nyumbani,
Kina mama kina baba, Mkotya mchagueni,
Tuachane na vibaba, Mkotya tumthamini,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Hana kiburi moyoni, ni mtendaji hakika,
Watu anawathamini, nayasema kwa hakika,
Uzuri ni hajivuni, kazini awajibika,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Tusimuache njiani, twende naye bila shaka,
Hakika ni tumaini, kamuinua Rabuka,
Na tuungane jamani, ushindi ni uhakika,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Wapinzani jishikeni, moto ameshauwasha,
Ameingia vitani, hakuna wa kumtisha,
Ni kubwa yake thamani, na Chemba anatutosha,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
Chemba hatuna mashaka, tunaye mtu makini,
Namaliza kuandika, nimesema si utani,
Twajivunia hakika, Mkotya ni mshindani,
Si mwingine ni Mkotya shujaa toka Mrijo.
SirDody (Mudio Islamic seminary)
Kilimanjaro , 0762396923 au 0675654955.
Post a Comment