HEADER AD

HEADER AD

MNYEKE TUMAINI LETU


MNYEKE ni tumaini, kwa watu wote Kondoa,

Jamii kaithamini, Kondoa kaiinua,

Nayasema si utani, jamii kaifikia,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Hakika kadhihirisha, kuitawala Kondoa,

Wajibu kakamilisha, kila mtu anajua,

Hakuna anayebisha, sifa tunakupatia,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Hana kiburi moyoni, ni mtendaji hakika,

Watu anawathamini, nayasema kwa hakika,

Uzuri ni hajivuni, kazini awajibika,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Tukatiki Oktoba, kwa jina lake Mnyeke,

Kina mama kina baba, tuthamini hadhi yake

Hakuna wa kuziiba, kura zote ni zakwake,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Tusimuache njiani, twende naye bila shaka,

Hakika ni tumaini, kamuinua Rabuka,

Na tuungane jamani, ushindi ni uhakika,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Msije mkasahau, ni Kondoa Vijijini,

Nawakumbusha wadau, Mnyeke mchagueni,

Msiwe vigeugeu, tumuweke akilini,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Wapinzani jishikeni, kwa moto wake Mnyeke,

Hakika ni mshindani, wa kwenu msimuweke,

Twamtaraji bungeni, twangoja ubunge wake,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.


Mwishoni nimefikia, mengi nimeelezea,

Mnyeke anatufaa, kwa jimbo kulichukua,

Shairi ninalitoa, mengi nimewahusia,

Mnyeke ni tumaini kwa watu wote Kondoa.

Chaguo la Mnyeke ni chaguo la maendeleo.


Tuchague mzalendo, mnyenyekevu na mchapakazi. Kondoa Vijijini – Ushindi ni Wetu!

Sir Dody – Mudio Islamic Seminary, Kilimanjaro)

 0762 396 923 | 0675 654 955

No comments