TMDA WATAKIWA KUFIKA VIJIJINI
Na Samwel Mwanga, Simiyu
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetakiwa kufika katika maeneo ya vijijini ili kutoa elimu, kufanya ukaguzi na kuhakikisha kuwa maduka ya dawa muhimu yanaendeshwa na watu wenye sifa stahiki, kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
Wito huo umetolewa Juni , 26, 2025 mjini Bariadi, katika kikao kazi kilichowakutanisha TMDA na wamiliki wa famasi na maduka ya dawa muhimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi wakiwa katika kikao na TMDA,mjini Bariadi.Wakizungumza kwenye kikao hicho, baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa wamesema kuwa hali ya upatikanaji wa wataalamu wa afya katika maduka ya vijijini bado ni changamoto kubwa.
Wamesema hali hiyo inayowalazimu baadhi ya watu kuendesha biashara hizo bila sifa zinazotakiwa kisheria.
Mmiliki wa duka la dawa mjini Bariadi Robart Mayongelo amesema “ Mfamasia aliyeidhinishwa ni nadra kupatikana vijijini. Maduka mengi yanaendeshwa na watu wasiokuwa na taaluma sahihi .
Robert Mayongelo ambaye ni mmiliki wa duka la dawa muhimu mjini Bariadi akizungumza na waandishi wa habari(hapo pichani)." Jambo linalohatarisha maisha ya wananchi. TMDA ifike kutoa mafunzo na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba ya mwaka 2019,” amesema Robert.
Naye Rose Makenge, mmiliki wa famasi mjini humo, alisisitiza umuhimu wa elimu kwa wauzaji wa dawa walioko vijijini.
“Tunahitaji TMDA kufika mara kwa mara vijijini, kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa kina ili kuhakikisha maduka yanaendeshwa na watu wenye sifa. Hii itasaidia wananchi kupata dawa bora na salama,” amesema.
Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Agrey Muhabuki, alikiri kuwapo kwa changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wa dawa maeneo ya vijijini na kueleza kuwa mamlaka hiyo imejipanga kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Agrey Muhabuki akizungumza katika kikao kazi kati ya wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi mjini Bariadi.“TMDA inatambua hali halisi vijijini. Tumejipanga kuendelea kutoa elimu na kushirikiana na wamiliki kuhakikisha wanazingatia matakwa ya kisheria. Lengo letu ni kulinda afya za wananchi,” amesema.
Ameongeza kuwa mamlaka hiyo inawahimiza wananchi kutoa taarifa wanapoona maduka yanayoendeshwa kinyume cha sheria ili hatua stahiki zichukuliwe kwa haraka.
Akifungua kikao hicho, Katibu wa Afya Mkoa wa Simiyu, Aziza Hamis, ameeleza kuwa wafanyabiashara wa dawa wamepewa dhamana kubwa na serikali hivyo ni lazima wazingatie sheria, kanuni na miongozo.
Katibu wa Afya mkoa wa Simiyu,Aziza Hamis akizungumza katika kikao kazi kati ya wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi mjini Bariadi.“Zipo changamoto nyingi kwenye baadhi ya maduka , wapo wanaolaza wagonjwa, kuchoma sindano au kufanya tohara, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za biashara ya dawa. Ni muhimu kila mmiliki akazingatia mipaka ya kazi zao,” amesema.
Kikao hicho kimeibua mjadala mpana juu ya udhibiti wa ubora wa huduma za afya kupitia maduka ya dawa na kutoa wito kwa TMDA kuongeza nguvu vijijini ambako uelewa bado ni mdogo na hatari kwa usalama wa wananchi kiafya.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi wakiwa katika kikao na TMDA,mjini Bariadi. Wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi mjini Bariadi wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji TMDA.
Post a Comment