WATANO WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
Na Alodia Dominick, Bukoba
MAHAKAMA kuu kanda ya Bukoba imewahukumu watu watano kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauji ya kukusudia Wilayani Ngara mkoani Kagera kwa nyakati tofauti.
Wakili wa Serikali Grolia Lugeye akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mashtaka mjini Bukoba alisema tukio la kwanza lilitokea Novemba mosi,2018 majira kati ya saa sita hadi saba usiku.

“Siku ya tukio majira ya usiku washitakiwa hao walienda nyumbani kwa Amosi Mfumu (80) ambaye ni marehemu na kuvunja mlango na baada ya kuingia ndani walikutana na mgeni ambaye alilala sebuleni aliyejulikana kwa jina la Mibulo Benedicto na kumuweka chini ya ulinzi.
"Wakati huo marehemu Amosi baada ya kusikia purukushani alitoka chumbani ndipo akakutana na wauaji hao na kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa”ameeleza Lugeye" amesema.
Amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo waliingia chumbani na kumuua pia mke wa marehemu Amosi ambaye aliitwa Solina Amosi (43) na kisha wakaiba simu ya Mibulo ambaye alikuwa mgeni.
"Kutokana na taa za mwanga wa jua zilizokuwa zikiwaka ndani Mibulo aliweza kuwatambua washitakiwa hao na kisha kutoa taarifa kwa majirani ambao walitoa taarifa kituo cha polisi na kufanikiwa kukamatwa.
Amesema kesi iliendelea kusikilizwa ambapo chanzo cha mauaji ni kwamba marehemu Amosi alihifadhi ng’ombe wake kwa Selemani Lwandindi ambapo alimtaka amrejeshee mifugo yake.
" Ndipo akajibiwa kuwa watarejeshewa lakini Selemani hakufanya hivyo badala yake aliwatafuta wauaji hao ambao ni Julius Ngeze,Jackson Bwelele na mwingine aliyeitwa Sadick alifariki wakati kesi ikiendelea.
Mahakama kuu kanda ya Bukoba ilisikiliza pande zote mbili na kulidhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri bila kuacha shaka lolote kuwa walifanya mauaji ya kukusudia ndipo ikawatia hatiani washitakiwa wawili.
" Washtakiwa hao ni Julius Ngeze na Seleman Lwandimdi na kuhumumiwa kunyongwa hadi kufa huku Jackson Bwelele akiachiwa huru kwani alitajwa na wenzake na mahakama iliona ushahidi dhidi yake haukujitoshereza.
Hukumu hiyo ilitolewa na jaji Lilian Itemba jaji wa mahakama kuu kanda ya Bukoba ambapo mawakili upande wa utetezi walikuwa ni Grolia Lugeye,Matrida Assey na Alice Mutungi ambao ni mawakili wa Serikali.
Katika tukio la pili Wakili Alice Mutungi amewataja washitakiwa Renatusi Misigalo (51),Mwendapole Andrea (44) na Kalenzo Ruhinda maarufu Ngaramandaje (54) wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua David Mbilahisha (52)kwa kukusudia.
“Washitakiwa hao walitenda kosa mnamo Januari 30,2017 katika kijiji cha Rulenge Wilayani Ngara ambapo siku hiyo majira ya usiku washitakiwa walifika nyumbani kwa David ambaye ni marehemu na kugonga mlango wakiwa na silaha zenye ncha kali ikiwemo panga huku, wakimuita mtoto wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Dickson David.
" Wakimtaka awafungulie mlango ambapo marehemu alitambua sauti ya Renatusi kwa kuwa walikuwa wanaishi kijiji kimoja na kwenda kumfungulia”ameeleza Mutungi.
Alisema baada ya kufungua mlango washitakiwa walimuweka David chini ya ulinzi na kumfunga kamba mikono na miguu,pia wakawachukua watoto watatu wa familia hiyo wakawafunga kamba mikono na miguu na kisha wakamuamuru marehemu awapatie fedha kwa sababu alikuwa ameuza shamba.
Alisema marehemu aliwajibu kuwa hana fedha ndipo wakaanza kutafunta wenyewe vyumbani na hawakupata chochote,wakaanza kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kufa baada ya kuona kafa waliiba televisheni moja na simu tatu za mkononi kisha kutokomea lakini watoto waliweza kuwatambua washitakiwa hao na walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge na washitakiwa kukamatwa.
Alisema Mahakama kuu kanda ya Bukoba baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka pasipo kuacha shaka lolote iliwatia hatiani washitakiwa hao wote watatu kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo ilitolewa Juni 13,mwaka huu na jaji Lilian Itemba jaji wa mahakama hiyo huku upande wa mawakili wa Serikali walioenedesha kesi hiyo wakiwa ni Agnes Awino,Grolia Lugeye na Alfred Tairo.
Katika tukio la tatu Wakili wa Serikali Alfred Tairo amesema mnamo Aprili 10,2024 katika kijiji cha Kilima Wilaya ya Bukoba ambapo Jovinary Godwin maarufu Muganyizi (16) na Editha Hermany maarufu Koku (47) walishitakiwa kwa kumuua mtoto Elias Antony (11).
Mwanafunzi huyo ni wa darasa la sita shule ya msingi Kilima ambapo siku ya tukio marehemu alikuwa na baba yake shambani wanachoma mkaa ambapo baba wa marehemu alimtuma mtoto aende nyumbani kuchukua unga,fedha na kisha apitie dukani ambapo baba aliacha simu kwa ajili ya kuongeza umeme.
“Marehemua alifanya kama alivyoelekezwa na baba yake lakini alichukua muda mrefu bila kurudi ambapo baba alimfuatilia bila mafanikio,Aprili 11 mwaka jana mwili wa marehemu ulipatikani ukiwa umekatwa na kitu chenye ncha kali shingoni ukiwa umetupwa kwenye eneo la tingatinga.
" Walifanikiwa kumkamata mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Jovinary ambapo alikiri kutekeleza mauaji hayo na kumtaja mshitakiwa wa pili Editha”ameeleza Tairo.
Amesema baada ya jaji Lilian Itemba wa mahakama kuu kanda ya Bukoba kusikiliza ushahidi uliotolewa alitoa hukumu ambapo Jovinary alipatikana na hatia lakini kwakuwa ni mtoto hakuhukumiwa kunyongwa.
Amerudishwa rumande mpaka Waziri wa katiba na sheria atakavyoona inafaa huku mshitakiwa wa pili Editha akiachiwa huru kutokana na ushahidi uliotolewa na mshitakiwa wa kwanza haukujitosheleza.
Post a Comment