MWANDISHI WA HABARI KIBAHA APENYA UDIWANI VITI MAALUM
Na Gustaphu Haule ,Pwani
MWANDISHI wa habari mkongwe kutoka gazeti la Uhuru Selina Msenga pamoja na wanawake wengine wanne wamefanikiwa kupenya katika uchaguzi wa udiwani wa Vitimaalum katika Manispaa ya Kibaha.
Msenga pamoja na wanawake wengine wameshinda katika uchaguzi wa umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Kibaha Mjini uliofanyika Julai 20, 2025 katika Kata ya Mkuza.
Katika uchaguzi huo Selina ambaye anatokea Tarafa ya Kibaha alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 527 akifuatiwa na Shufaa Bashari aliyepata kura 581 huku Aziza Mruma akipata kura za kishindo 952.
Mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru Selina Msenga wa tatu kutoka kulia akiwa na washindi wenzake mara baada ya kutangazwa kuwa washindi katika uchaguzi wa UWT Kibaha Mjini uliofanyika Julai 20,2025.
Wengine kutoka Tarafa ya Kongowe aliyeshinda ni Sara Uled aliyepata kura 864 na Lidya Mgaya aliyefanikiwa kutetea nafasi yake kwa kupata kura 575.
Kibwana amesema kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na wagombea 15 huku wapiga kura wakiwa 1094 na kusema kura halali zilikuwa 1083 huku kura zilizoharika ni 11.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi na aliyetangaza matokeo ni Ally Kibwana ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo.
Kibwana amewashukuru wajumbe hao kwa uvumilivu na utulivu wao hali ambayo ilisababisha uchaguzi huwe huru ,utulivu na amani na kuwataka wajumbe hao kuendelea kushikamana zaidi katika chaguzi zijazo.
Washindi wa uchaguzi wa udiwani viti maalum Kibaha Mjini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa katika uchaguzi uliofanyika Julai 20,2025.
Aidha Kibwana ametaja majina ya wagombea wengine walioingia katika kinyang'anyiro hicho na Tarafa zao kuwa katika Tarafa ya Kibaha ni Magreth Fabian(55),Joyce Francis (74),Rehema Abdallah (103), Beatrice Manyama (192),Emiliana Damson(294),na Maria Msimbe (420).
Katika Tarafa ya Kongowe ni Beatrice Kessy(99), Elizabeth Nyambilila (113),Mariam Gama(180) na Tatu Kondo (343).
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Halima Dossa amewashukuru wagombea kwakuwa na moyo wa ujasiri ambaye alisema kuwa huo ndio uanasiasa na haitakiwa kwenda katika uchaguzi na matokeo mfukoni
Hata hivyo, Dossa amewashukuru wanafunzi waliojitokeza kusaidia uchaguzi huo ambapo amesema wawe na moyo huo na kwamba imani yake watakuwa wanasiasa wazuri baadaye.
Mshindi wa kwanza katika uchaguzi wa udiwani wa Vitimaalum uliofanyika jana Julai 20,2025 Aziza Mruma wa Kwanza kushoto,Shufaa Bashari wa pili na watatu Selina Msenga.
Post a Comment