MUSSA NSEKELA AIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI JIMBO LA KYERWA

Na Alodia Dominick, Kyerwa
MJUMBE wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Khald Mussa Nsekela ameongoza kura za maoni katika jimbo la Kyerwa kwa kupata kura 5693 kati ya kura 8,134 zilizopigwa.
Katibu wa CCM Wilaya hiyo Kisamba Kisando ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi akitangaza matokeo hayo amewataja wagombea wengine kuwa ni
Innocent Bilakwate aliyekuwa mbunge kwa hawamu iloyopita ambaye amepata kura 1567,Stephen Katemba kura 542 na Maxson Baritazary kura 152.
Amewataja wengine kuwa ni Benedicto Mutungilehi kura 101 na Sperata Marco aliyepata kura 16 .
Amesema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 8420 waliojitokeza kupiga kura ni 8134 zilizoharibika ni kura 63 na kura halali ni 8071 hivyo kumfanya Khald Nsekela kuongeza katika katika uchaguzi huo.
Post a Comment