MHANDISI MUTASINGWA AIBUKA MSHINDI KURA ZA MAONI UBUNGE BUKOBA MJINI

Na Alodia Dominick, Bukoba Mjini
MHANDISI Jonston Mutasingwa ameongoza katika kura za maoni Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 1,408 katika jimbo la Bukoba mjini mkoani Kagera.
Mhandisi Mutasingwa amepata kura nyingi dhidi ya wenzake wanne na hivyo kuwa wa kwanza baada ya kupigiwa kura za maoni na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Bukoba Mjini.
Mhandisi Jonston Mutasingwa akiwashukuru wanaccm wa Bukoba mjini kwa kumpa kura nyingi.Akitangaza matokeo Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini ambaye pia ni katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bukoba Mjini Shaban Mdoe amemtangaza Mhandisi Mutasigwa kuwa ndiye wa kwanza kwa kupata kura nyingi 1,408 katika jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bukoba Mjini ambaye pia ni katibu wa CCM Bukoba mjini Shaban Mdoe akitangaza uchaguzi."Wajumbe waliojiorodhesha kupiga kura walikuwa 3,033, kura zilizopigwa ni 2,978, kura zilizoharibika 20 kura harali 2,958" amesema Mdoe
Amewatangaza wengine waliopigiwa kura kuwa Mwl. Koku Ruta aliyepata kura 40, Mwl. Jamila Emily aliyepata kura 66, Almasoud Kalumuna kura 640 na Alex Muganyizi kura 804.
Post a Comment