HEADER AD

HEADER AD

RWEIKIZA AIBUKA MSHINDI KURA ZA MAONI UBUNGE BUKOBA VIJIJINI


Na Alodia Dominick, Bukoba Vijijini

MBUNGE wa Jimbo la Bukoba vijijini aliyemaliza muda wake ambaye anatetea  nafasi yake, Jasson Rweikiza ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 6,465.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bukoba Vijijini ambaye pia ni katibu wa chama Jesca Ndyamukamu amemtangaza Rweikiza kuwa mshindi kwa kuwashinda wagombea wenzake watano na yeye kuibuka mshindi katika nafasi hiyo kwa kupata kura 6,465.

Mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM jimbo la Bukoba Vijijini Jesca Ndyamukama akitangaza matokeo ya kura za maoni katika jimbo hilo.

"Wagombea walikuwa sita kura zilizopigwa 11,682, kura zilizoharibika 100, kura harali 11,582" amesema Ndyamukama

Wagombea wengine waliopigiwa kura ni Filbert Bagenda amepata kura 44, Edmund Lutaraka kura 89, Asted Mpita kura 124, Fahami Matsawile kura 239, Faris Burhan kura 4,619.

       Mbunge anayetetea kiti chake Jasson Rweikiza ambaye amekuwa wa kwanza katika kura za maoni jimbo la Bukoba vijijini.

      Baadhi ya wananchi wakimsikikiza mkurugenzi wa uchaguzi.

No comments