USHINDI TWAWATAKIA
KIUME kapambaneni, matokeo twayataka,
Chezeni kwa umakini, mtashinda kwa hakika,
Nafasi zitumieni, ushindi utasikika,
Twawatakia ushindi timu yetu ya Taifa.
Ni michuano ya chani, inafanyika nchini,
Timu yetu miongoni, tutaiona dimbani,
Timu ngeni karibuni, Tanzania ya amani,
Twawatakia ushindi timu yetu ya Taifa.
Kwa mkapa kutawaka, nyasi zitalalamika,
Mpira utapigika, watu watafurahika,
Timu yetu kwa hakika, mshindi itaipuka,
Twawatakia ushindi timu yetu ya Taifa.
Mwishoni nimefikia, ushindi twasubiria,
Mengi nemeelezea, timu yetu kusifia,
Shairi ninalitoa, kwa heri kuwatakia,
Twawatakia ushindi timu yetu ya Taifa.
SirDody, 0675654955
Post a Comment