HEADER AD

HEADER AD

UZALENDO NI WAJIBU KWA VIONGOZI

UZALENDO ndo kujituma, na kwa nchi kujitoa, 

Kuyaendeleza mema, kwa watu kuwatetea, 

Kutenda bila dhuluma, na haki sawa kutoa, 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


Nchi itumikieni, kwa hekima na busara, 

Jamii ithaminini, hilo litakuwa bora,

Idumisheni amani, sisababishe hasara,

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


Changamoto tatueni, kwa wananchi muhimu, 

Nchi yenu ipendeni, idumisheni nidhamu, 

Malumbano ofisini, kwa Taifa si muhimu, 


Na rushwa jiepusheni, ni hatari maishani,

Ongozeni kwa yakini, kwa nidhamu na imani,

Madaraka sitamani, nayasema si utani, 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


Umepewa madaraka, watu wakakuamini, 

Yatumie kwa hakika, kwa watu kuwathamini, 

Wasije wakakuchoka, wakakuona mhuni, 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


Katiba simamieni, sije ivunja sheria, 

Nchi imewaamini, kwa huduma kuzitoa, 

Na wizi jiepusheni, serikali kuibia, 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


Namaliza kuandika mengi nimewahusia, 

Mengi nimeyaandika, ni kazi kuyafanyia,

Kukumbusha sitochoka, kwa ujumbe kuutoa, 

Viongozi wazalendo ni muhimu kwa Taifa. 


*SirDody

_Mudio islamic Seminary_.

Moshi Kilimanjaro

0762396923 au

0675654955

No comments