HAWA MCHAFU AELEZA MAKUBWA YALIYOFANYIKA JIMBO LA KIBAHA VIJIJINI
Na Gustaphu Haule,Pwani
MBUNGE mteule wa Vitimaalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu ameshiriki katika uzinduzi wa kampeni za CCM Jimbo la Kibaha Vijijini na kusema yupo tayari kupita Kata zote 14 za Jimbo hilo kwa ajili ya kumuombera kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea wa ubunge Hamoud Jumaa.
Mchafu amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini,Mkoa,Taifa ,Wanachama wa CCM na Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni hizo Septemba 19/205 katika viwanja vya Kata ya Mtongani vilivyopo Mjini Mlandizi.
Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akizungumza na Wananchi pamoja na wanachama wa CCM katika uzinduzi wa Kampeni za ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini zilizofanyika Septemba 19,2025 katika viwanja vya Kata ya Mtongani Mjini Mlandizi Kibaha Pwani.
"Nitazunguka Kata zote 14 kwa ajili kuunganisha nguvu na madiwani kuomba kura za Dkt . Samia ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwake kwa kile ambacho Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan amekifanya katika Jimbo la Kibaha Vijijini,", amesema Mchafu.
Mchafu amesema kuwa Dkt.Samia ndani ya miaka minne tangu alipochukua kijiti amefanya mambo makubwa ya maendeleo Jimbo la Kibaha Vijijini.
Amesema katika kipindi hicho Dkt.Samia ametoa zaidi ya Sh. Bilioni 6.32 kujenga jengo la utawala na nyumba ya mkurugenzi na katika upande wa elimu msingi ametoa Sh .Bilioni 289 kwa ajili kujenga shule tatu za msingi na awali.
Ametaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule ya Constantine Mwakamo,MwembeNgozi na Mkombozi lakini hatahivyo kwa upande Sekondari Dkt .Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya Sh.bilioni 3.5 .
Kuhusu afya amesema Dkt.Samia ametoa sh.Bilioni 354 kwa ajili ya kukarabati na ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya ambayo kwasasa inatumika kuwahudumia Wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Pia ,Mchafu amesema amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwawekea mazingira akina mama wenzake kuhakikisha wanaacha kutumia nishati chafu na akamua kutoa Nishati Safi ya kupikia.
Mchafu amesema Rais Samia ametoa majiko ya gesi kwa akina mama,baba lishe na wajasiriamali mbalimbali ili waweze kufanya shughuli zao kirahisi zaidi pamoja na kuboresha mikopo ya asilimia 10.
Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu ( wa pili kutoka kushoto) akiwa katika uzinduzi wa kampeni za ubunge Jimbo la la Kibaha Vijijini zilizofanyika Septemba 19,2025 katika viwanja vya Mtongani Mlandizi.
Amesema mikopo ya asilimia 10 imewasaidia akina mama waondokane na mikopo ya kausha damu na mikopo ya nguo za mkononi na kwamba katika mikopo hiyo asilimia nne zinaenda kwa akina mama, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili zinaenda kwa walemavu.
Amesema hakuna kitu cha kumlipa Rais Samia zaidi ya kuhakikisha ifikapo Oktoba 29,2025 wananchi wote waende wakapige kura kwa Rais Samia ikiwa ni sehemu ya kumpa heshima kwa yale aliyoyafanya.
Amesema pia yupo mbunge ( Mzee wa Sambusa) Hamoud Jumaa ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa miaka 10 na sasa amerudi tena na kusema Mbunge huyo anauzoefu wa kutosha ni sawa na Samaki aliyerudi baharini .
Hata hivyo Mchafu amewaomba Wananchi hao kuhakikisha Oktoba 29, wanaungana kuwapigia kura madiwani wote wa CCM na mbunge huyo ilikusudi wakafanyekazi pamoja na Rais ya kuwaletea maendeleo Wananchi.



Post a Comment