HEADER AD

HEADER AD

MBUNGE MSTAAFU KIBAHA AWATAKA WANACCM KUACHA VIJEMBE DHIDI YAKE

Na Gustaphu Haule, Pwani

MBUNGE mstaafu wa Jimbo la Kibaha Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Michael Mwakamo amekunjua makucha na kuwataka baadhi ya  viongozi wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini kuacha vijembe dhidi yake kwakuwa huu sio muda wake bali ni muda wa kutafuta kura kwa ajili ya ushindi wa chama.

Mwakamo ametoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano wake maalum alioutisha kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali ya kisiasa mara baada ya kamati Kuu ya CCM kumteua Hamoud Jumaa kugombea ubunge wa Jimbo hilo.

         Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo ( CCM) akiwa katika mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika juzi Mlandizi Kibaha Vijijini.

Mwakamo ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 alikuwa ametetea nafasi katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika Agosti 4 mwaka huu lakini kura zake hazikutosha na hatimaye Hamoud Jumaa kuongoza kwa zaidi ya kura 3000 huku Mwakamo akipata zaidi ya kura 1000.

Mwakamo,amesema kuwa katika mchakato wa uchaguzi wa kura za maoni yeye jina lake lilirudishwa akiwa pamoja na Hamoud Jumaa na Heri Achahofu lakini kwa upande wake kura hazikutosha na hatimaye kukosa nafasi ya kugombea ubunge katika Jimbo hilo.

Amesema ,yeye hapingani na utaratibu wa chama kwakuwa CCM inautaratibu wake na bado kuna nafasi nyingi ambazo mtu anaweza kugombea na akapata lakini shida ipo kwa viongozi wa chama wa Jimbo hilo.

Amesema wapo baadhi ya viongozi licha ya jina lake kutoteuliwa lakini wamekuwa na kauli za kejeli dhidi yake ikiwa na  kumtengenezea maneno ya kusudio lake la kuhama chama jambo ambalo linaleta mpasuko wa kisiasa.

Amewaomba viongozi wenye tabia hizo waache tabia hiyo kwani muda huu wanatakiwa kushirikiana katika kutafuta kura za Rais, mbunge na madiwani na kwamba yeye hana nongwa ya aina yoyote.

Amesema kwa wanaodhani anataka kuhama chama hizo ni fikra zao na hawezi kuwazuia kuongea lakini anachojua yeye ni mwanaCCM aliyezaliwa katika familia ya CCM na wala hafikirii kuhama chama.

"Nawaomba waandishi wa habari mnisaidie kufikisha ujumbe huu kwa Watanzania kuwa mimi Michael Mwakamo sina mpango wa kuhama chama isipokuwa wapo watu wanazusha maneno hayo na hajawatuma kufanya hivyo,"amesema Mwakamo 

Ameongeza kuwa muda huu ni muda wa kampeni na hakuna haja ya malumbano na kwamba watu wanaomuunga mkono wasifuate maneno yenye fitina bali wamsikilize yeye.

Amesema anakishukuru Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wanaCCM wa Jimbo la Kibaha Vijijini kwa kumuamini katika kipindi cha miaka mitano ikiwa tangu 2020 hadi 2025 lakini pia anawashukuru Wananchi kwa kumpa heshima ya kubwa mbunge.

Amesema kipindi hicho Kibaha Vijijini walikuwa na idadi ya Wananchi 24,000 na aliweza kupata kura 21,000 lakini anamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani alipokuwa anapeleka changamoto za jimbo lake zilikuwa zinafanyiwa kazi.

Amesema katika kipindi chake amefanya mambo makubwa katika Jimbo lake na alitamani kuona anafanya makubwa zaidi ndani ya miaka mitano ijayo lakini ndoto zake zimefifia japo anaamini hata yule anayeingia ataweza kufanya vizuri zaidi.

Amesema baada ya matokeo kutoka watu wenye mapenzi ya dhati walilala ndani na wengine walikuwa wakiumwa ambapo amewatoa hofu watu wake kuwa ameyapokea matokeo hayo kwa kufuraha .

Hatahivyo,amesema pamoja na kuwepo kwa kejeli dhidi yake lakini yeye kwa heshima aliyonayo yupo tayari kushiriki kampeni zote kwa ajili ya kuomba kura lakini atakuwa mtu wa ajabu kususia chama.

No comments