HEADER AD

HEADER AD

MGOMBEA UBUNGE KYERWA ALIA NA VITAMBULISHO VYA NIDA

Na Alodia Dominick, Kyerwa

MGOMBEA ubunge jimbo la Kyerwa  Khalid, Mussa Nsekela amemuomba mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi kusaidia upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA).

amesema kuwa chama hicho kitakaposhika dola kisaidie kutatua changamoto inayowakabili wananchi wa jimbo hilo ya kukosa vitambulisho vya Taifa (NIDA). 

Nsekela ametoa ombi hilo baada ya Dk.Nchimbi kumnadi kwa kuwahakikishia wananchi kuwa mgombea huyo anafaa na atawaletea maendeleo.

Kampeni hizo zimefanyika leo katika viwanja vya stend ya mabasi Nkwenda wilayani Kyerwa.

        Mgombea mwenza nafasi ya Urais akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kyerwa Khalid Mussa Nsekela katika  stend ya magari Nkwenda.

Nsekela amewaomba wananchi wa jimbo la Kyerwa itakapofika Oktoba, 29 mwaka huu kupiga kura kwa wagombea wa chama cha mapinduzi (CCM) kupiga kura kwa ajili Rais, wabunge na madiwani.

"Nashukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama yetu Dk.Samia amefanya na kutekeleza mengi sisi sote ni mashuhuda.

"Pia anaendelea kutuahidi mengi ambayo anakwenda kuyatekeleza naomba ili wananchi hawa wanufaike na fursa hizo, Dkt. Nchimbi naomba msaada wako wananchi wanahitaji Nida" amesema.

Amesema wananchi wanakosa huduma za msingi ikiwemo mikopo kwa ajili ya kujiletea maendeleo hivyo hiyo ni changamoto kubwa katika eneo hili.

     Wananchi waliohudhuria mkutano wa Kampeni.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kyerwa Daniel Damian amemwakishia mgombea mwenza  wa nafasi ya Urais (CCM) kuwa chama hicho kitashinda kwa kishindo katika jimbo.

Amesema kuwa jimbo hilo lina kata 24 kata tisa ndizo zimekuwa na wapinzani waliochukua fomu na kata 15 madiwani wake watapigiwa kura za ndiyo na hapana.

Naye mgombea mwenza wa kiti cha Urais Balozi Emmanuel Nchimbi amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

        Mgombea mwenza nafasi ya Urais akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kyerwa Khalid Mussa Nsekela katika  stend ya magari Nkwenda.

Serikali itaboresha hospitali ya wilaya ya Kyerwa, vituo vya afya vitano, kujenga shule mpya za sekondari nne, ahile za msingi saba.

Miradi mingine itakayojengwa ni pamoja na visima vipya vya maji kutoka visima 334 hadi 426, kuongeza skimu za umwagiliaji kutoka 15 hadi 17.

    Wananchi waliohudhuria mkutano wa Kampeni

No comments