RC PWANI AWAAGIZA WATOA MIKOPO KUTOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA
Na Gustaphu Haule, Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewaagiza wataalam wanaoshughulikia masuala ya mikopo kwa wafanyabiashara wadogo kuhakikisha wanatoa elimu ya biashara kwa wahusika ili kuwasaidia katika kukuza na kuimarisha biashara zao.
Aidha , Kunenge amewataka pia kufanya tathmini ya kuonesha mafanikio ya wafanyabiashara waliochukua mikopo huku akisema hatua hiyo itakuwa njia ya kumtia moyo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa fedha kwa wafanyabiashara hao.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akifungua kongamano la wafanyabiashara wadogo wa Mkoa wa Pwani lililofanyika Septemba 8,2025 Mjini Kibaha.Kunenge ametoa maagizo hayo wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara wadogo wa Mkoa wa Pwani lililofanyika Septemba 04,2025 katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa Pwani .
Alisema Rais Samia amefanyakazi kubwa ya kuwapigania wafanyabiashara wadogo ndio maana kwasasa kumekuwa na mikopo ambayo inatolewa na Serikali na yenye riba nafuu.
Amesema Serikali inataka kuona namna Wananchi wake wanavyonufaika na mikopo hiyo ndio maana kila mara imekuwa ikiweka mipango madhubuti ya kukuza na kuimarisha biashara zao.
Baadhi ya wawezeshaji wa taasisi wezeshi za Serikali wakiwa mstari wa mbele katika kongamano la wafanyabiashara lililofanyika Septemba 8,2025 Mjini Kibaha.Amesema haiwezekani Serikali kupitia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inatenga fedha nyingi za mikopo kwa wafanyabiashara wadogo halafu walengwa hawajui jambo ambalo lazima liwekewe mikakati.
"Wataalam lazima mtoe elimu ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo na ikiwezekana wafanye tathmini ya kujua hatua za maendeleo zilizofikiwa na wafanyabiashara hao tangu walipoanza kuchukua mikopo ,"amesema Kunenge
Kunenge amewaagiza wafanyabiashara wadogo kuhakikisha wanapochukua mikopo hiyo lazima wajue kurejesha mikopo hiyo ndani ya muda ili kutoa nafasi kwa wengine kunufaika.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema,amesema kuwa Mkoa umekuwa ukiendesha zoezi la usajili wa wafanyabiashara wadogo ambapo kwasasa waliosajiliwa ni 4,183 wakiwemo Wanawake 3,306 na Wanaume ni 1,507 ambapo kati yao walipata vitambulisho ni 1,345.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema katika kongamano la wafanyabiashara wadogo lililofanyika Septemba 8,2025 Mjini Kibaha.Mnyema amesema anaishukuru Serikali kwa kazi kubwa iliyofanya hasa katika kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wadogo ikiwemo kutoa fedha za mikopo yenye riba nafuu na kwamba kinachotakiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wanachangamkia fursa hiyo.
Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Pwani Philemon Maliga,amemshukuru Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyopambana na vitu vitatu ikiwemo ujinga,malazi na umaskini na kwamba hata wao kwasasa wamekuwa wakichangia mapato ya Taifa kwakuwa tayari Rais amewatengenezea mazingira rafiki.
Amesema anamshukuru Rais Samia kwakuwa amefanikisha kuwajengea Machinga ofisi ya Mkoa wa Pwani na hata kuwatambua wamachinga na kuwasajili ambapo amewasisitiza wamachinga wenzake kujisajili kwakuwa Serikali haiwezi kumsaidia mtu asiye hitaji.
Nae Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Machinga Taifa Sili Usile amemshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuwainua machinga hapa nchini japokuwa bado kuna changamoto ya namna ya utoaji wa mikopo hiyo.
Usile amesema kuwa changamoto ya kwanza ni kwamba mikopo hiyo inatolewa kulingana na makazi na biashara ya mtu husika kwani wapo watu wanaishi Kibaha lakini wanafanyabiashara Dar es Salaam akisema mtu kama huyo hapati mkopo.
Changamoto nyingi ni kuhusu vitambulisho vya ujasiriamali ambapo amesema vitambulisho hivyo uchelewa kutolewa kwani wapo watu wamejisajili Machi mwaka huu lakini hadi leo hawajapata vitambulisho.
Changamoto nyingine ni kuwa Rais Samia kuwa ametoa fedha nyingi za Wamachinga lakini watu wa Benki ambao wamepewa jukumu la kutoa fedha hizo ndio kikwazo kwakuwa wamekuwa na masharti mengi ambayo hayana msingi.
Wafanyabiashara wadogo wakiwa katika kongamano lao lililofanyika Septemba 8,2025 Mjini Kibaha.Mwakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Grace Mwikola amesema Wizara inawatambua wafanyabiashara wadogo kuwa ni wale wenye mitaji ya kuanzia Sh.10,000 hadi Sh.milioni 4.
Amesema kupitia kongamano hilo ni vyema wafanyabiashara wakashirikiana ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mtu anajisajili kwa kupata kitambulisho cha ujasiriamali ili aweze kufaidika na fursa hizo.
Hatahivyo Mwikola amesema katika kongamano hilo amepokea changamoto na ataziwasilisha Wizarani ili kusudi ziweze kufanyiwa kazi huku akiwasisitiza wajasiriamali kuwa na vitambulisho vya machinga.
Post a Comment