RC PWANI AZINDUA UGAWAJI WA VYANDARUA
>> Mkurugenzi Sungusia asema lengo ni kutekeleza mpango mkakati wa Serikali wa kupambana na Malaria
Na Gustaphu Haule, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezindua ugawaji vyandarua kwa wananchi wa mkoa wa Pwani huku akiwataka Wananchi watakaopewa vyandarua hivyo kuvutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kunenge,amezindua mpango huo Septemba 09/2025 hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani iliyopo Kibaha Mjini hafla ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (katikati)akizindua mpango wa ugawaji vyandarua kwa Wananchi uliofanyika Septemba 09,2025 Mjini Kibaha na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Ugavi na Uendelezaji wa MSD Victor Sungusia.Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Bohari ya madawa ( MSD) Kunenge amewataka wananchi kuacha kutumia vyandarua hivyo kuweka uzio wa vifaranga vya kuku na kuvulia samaki,kuweka uzio katika bustani na katika matumizi mengine tofauti na makusudio.
Kunenge amesema Malaria ni ugonjwa ambao unaleta madhara kiuchumi na kwa watoto na hivyo kila mmoja anatakiwa kuhakikisha analinda maisha yake kwa kuondoa ugonjwa huo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (Kulia) katika zoezi la uzinduzi wa mpango wa ugawaji vyandarua kwa Wananchi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Pili Mnyema."Tunatakiwa kuhakikisha tunaondoa malaria kwa kuweka maeneo safi na kutumia vyandarua,tusitumie vyandarua hivi kinyume cha utaratibu kufugia kuku na kuvulia samaki",amesema.
Kunenge pia amewahakikishia wananchi kwamba vyandarua hivyo havina madhara yoyote kwakuwa vimepitia taratibu zote na vinaviwango vya kimataifa na wasisikilize taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu wachache.
Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji kutoka Bohari ya Dawa (MSD) Victor Sungusia amesema kuwa mpango wa ugawaji vyandarua hivyo upo chini ya Bohari ya madawa nchini( MSD) na ugawaji wa vyandarua hivyo ni katika kutekeleza mpango mkakati wa Serikali wa kupambana na Malaria.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizindua mpango wa ugawaji vyandarua kwa Wananchi hafla ambayo imefanyika Septemba 09,2025 katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani.Amesema katika utaratibu wa ugawaji wa vyandarua hivyo mkoa wa Pwani ni mkoa wa tatu na awali tayari wamegawa vyandarua hivyo katika Mkoa wa Shinyanga na Kigoma na kwamba baada ya Mkoa wa Pwani wataendelea na Mikoa mingine Saba.
Sungusia amesema hadi sasa vyandarua milion 40 tayari vimegawiwa kwa Wananchi na kwa mkoa wa Pwani vyandarua 1,200,000 vitagawiwa kwa kaya zilizoainishwa ndani ya siku 21.
Sungusia ametoa wito kwa Wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili kuhakikisha wanafikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Dr. Kusirye Ukio amesema kaya 494,595 zimetembelewa sawa na asilimia 110 ambazo zina watu 2,228,485 na zimetambuliwa kwa ajili ya utaratibu wa kugawiwa vyandarua hivyo.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Pwani Kusirye Ukio akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa ugawaji vyandarua uliofanyika Septemba 09,2025 Mjini Kibaha.
Post a Comment