HEADER AD

HEADER AD

MUSEVENI AANDALIWA AWAMU YA SABA, UPINZANI WAGAWANYIKA


Kauli ya kiongozi mmoja wa upinzani nchini Uganda kwamba Rais Museveni hawezi kushindwa katika uchaguzi mkuu imezusha mjadala mkali Uganda.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Wakati Rais Yoweri Museveni wa Uganda akijiandaa kuteuliwa tena kuwania kiti hicho cha urais kwa awamu ya saba, tamko la kiongozi mmoja wa upinzani kwamba kiongozi huyo hawezi kushindwa katika uchaguzi limeibua maoni mseto.

Viongozi wengine wa upinzani wanaelezea tamko hilo kuwa njia ya kuwavunja moyo Waganda wasitarajie chochote cha maana katika uchaguzi mkuu ujao kama njia ya kushiriki utawala wa kidemokrasia.

Kulingana na kiongozi huyo Norbert Mao rais wa chama kikongwe cha DP ambaye pia kwa sasa ni waziri wa masuala sheria na katiba, vyama vitano vya upinzani vimeungana na chama tawala kujadili mchakato wa mapito ili Rais Yoweri Museveni aachie madaraka kwa njia ya amani.

Kwa kauli yake, vyama vya upinzani ambavyo vimesusia kushirikiana na chama tawala ndivyo vinachelewesha kung'atuka kwa Museveni ambaye ameongoza Uganda kwa takriban miaka 40.

Mwanasiasa wa upinzani Uganda, Kizza Besigye
Dr. Kizza Besigye, mwanasiasa mkongwe na mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Uganda inajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka 2026, huku sehemu ya upinzani ikilalamika kutishiwa.

Norbert Mao ameorodhesha vyama vitano vya upinzani pamoja na vuguvugu la mwanawe Museveni jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa muungano wenye nguvu zaidi unaomuunga mkono rais Yoweri Museveni na wako tayari kujadili naye kuhusu utawala wa mpito ili aachie madaraka kwa amani.

"Unaweza kuliita kundi la vyama vitano na ni kundi kubwa. Na lile kundi lingine ni kundi ambalo haliwezi kuaminiwa kukabidhiwa madaraka kwani madaraka si ya kila mtu ndiyo maana nawambia makabidhiano ya madaraka hayatatokana na uchaguzi," amesema Mao.

Lakini tamko lake limepokelewa kwa maoni ya ghadhabu na mshangao na watu mbalimbali kuanzia raia wa kawaida hadi viongozi wa upinzani.

 Rais wa chama kikuu cha upinzani NUP Robert Kyagulanyi yaani Bobi Wine ametaja tamko hilo kuwa la kupotosha katika hatua ya kuwavunja moyo wafuasi wa vyama vingine vya upinzani na kuonya kwamba watapinga kabisa mwelekeo huo.

"Ni jambo la kusikitisha kuwa kiongozi wa chama cha DP ambaye wakati mmoja alijulikana kuna na busara akitoa tamko kama hilo. Atashangaa kwani hautakuwa uchaguzi kimya tutafanya kila hila kutasema na  kupiga mayowe," amesema Kyagulanyi.

     Rais wa chama kikuu cha upinzani NUP Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) ametaja tamko la Mao kuwa la kupotosha.
Picha

Wakati huohuo, waziri wa masuala ya ndani ya nchi Jenerali Kahinda Otafire amehoji kwa nini upinzani ukoseshwe fursa za kushiriki shughuli za kidemokrasia pale viongozi na wafuasi wanapokamatwa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu baada ya wao kujitokeza kugombea nafasi za kisiasa.

Ametoa mfano wa kiongozi mkongwe wa upinzani Dkt Kizza Besigye ambaye kesi dhidi yake imedorozwa na kumsababisha kushindwa kushiriki uchaguzi akiwa mshika bendera wa chama chake cha PFF.

"Sidhani kama ni haki kuendelea kuwakandamiza watu hao. Dkt Kizza Besigye hana hatia katika mahakama ya umma," amesema Besigye

Wiki ijayo Jumanne, Rais Museveni anatarajiwa kuteuliwa na tume ya uchaguzi kuwania urais. Bobi Wine naye amesema anataka kuteuliwa siku hiyo hiyo.

Chanzo : DW


No comments