HEADER AD

HEADER AD

WATU SITA WAFA PAPO HAPO KWA AJALI YA GARI BUKWE



>> Watu hao walikuwa wakienda Mwalo wa Busurwa 

DIMA Online

WATU sita (6) ambao bado hawajatambulika majina yao waliokuwa wakitoka wilaya ya Tarime wakisafiri kwenda Mwalo wa Busurwa , wilayani Rorya mkoani Mara, wamefariki papo hapo baada ya gari walilokuwemo kupata ajali baada ya kuiparamia fuso iliyoharibika iliyokuwa limepaki barabarani.

Tukio hilo limetokea Tarehe 11, Septemba , 2025, majira ya saa kumi na dakika 50 ( 4: 50 AM ) alfajiri katika Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya ambapo marehemu walikuwa kwenye gari  ndogo yenye namba za usajili T.625 DYV aina ya Probox huku majeruhi mmoja akikimbizwa hospitali kwa matibabu .

            Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo katika Kijiji cha Kongo kata ya Bukwe wilayani Rorya.

Gari hilo aina ya Probox ililigonga kwa nyuma Fuso yenye namba za usajili T. 857 BRX Mitsubishi iliyokuwa ikielekea Musoma ambayo iliharibika ikaegeshwa barabarani katika eneo hilo la Kongo bila tahadhari.


No comments