HEADER AD

HEADER AD

CWT SIMIYU YAKANUSHA WALIMU KUZUILIWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

Na Abdallah Nsabi, Simiyu

CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) mkoani Simiyu, kimekanusha barua inayosambaa mitandaoni  juu ya walimu kutoshiriki uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa chama hicho, mkoa wa simiyu, mwalimu mathias sinzika akizungumza na waandishi wa habari amesema barua hiyo inapaswa kupuuzwa haijatoka chama cha walimu( CWT).

        Mwenyekiti wa Chama cha walimu mkoa wa Simiyu Mathias Sinzika aizungumza.

Amesema chama cha walimu kitashiriki zoezi la uchaguzi kwa kila kitu ikiwemo upigaji wa kura octoba 29 mwaka huu.

Amewasisitiza wananchi hususani walimu kupuuza barua hiyo ambayo imetengenezwa kwa lengo la kuwachonganisha walimu na serikali yao.

Pia mwenyekiti huyo amewaomba walimu na wananchi kushiriki uchaguzi ikiwemo upigaji wa kura.

No comments