RC PWANI AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA
Na Gustaphu Haule, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewaomba wananchi waliopo ndani ya mkoa wake kujitokeza kwa wingi kushiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 /2025.
Kunenge ametoa wito huo Oktoba 27 /2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake ambapo lengo kubwa lilikuwa ni kuzungumzia hatua za mwisho za maandalizi ya Uchaguzi mkuu.
Amesema maandalizi yote yamekamilika hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kushiriki kupiga kura kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
Kunenge amesema Mkoa huo uko salama na umejidhatiti kuhakikksha hakuna mtu yeyote atakayethubutu kuvuruga uchaguzi kwahiyo wananchi wasiogope wala kutishwa na mtu .
"Vyombo vya usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha usalama umeimarishwa hakuna mwananchi atakayesumbuliwa, kutishwa wala kuzuiwa kupiga kura kwahiyo wote waende kupiga kura wakiamini hali ya usalama upo vizuri," amesema Kunenge .
Kwa mujibu wa Kunenge Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 3,941 vya kupigia kura ambavyo vimewekwa karibu na maeneo ya makazi ya wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 27 kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29/2025.Naye Afisa uchaguzi Jimbo la Kibaha Vijijini Grace Haule akizungumzia maandalizi ya vituo kwenye jimbo hilo ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi kwa kuwapatia vifaa kwa wakati.
Haule amesema jimbo hilo lenye vituo 267 na mandalizi yake yamekamilika ambapo amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuzingatia muda.



Post a Comment