LUGOMELA AFUNGA KAMPENI KWA KISHINDO JIMBO LA MASWA MASHARIKI
Na Abdallah Nsabi , Simiyu
MGOMBEA Ubunge jimbo la Maswa mashariki, mkoani Simiyu kupitia Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt. Georgr Lugomela amewaahidi wakazi wa maswa Mashariki iwapo watamchagua wilaya itakuwa ya mfano kwa maendeleo.
Akihitimisha kampeni za ubunge jimbo la Maswa Mashariki uwanja wa Madeco kata ya Shanwa mjini Maswa amesema jimbo la Maswa mashariki litakuwa la mfano kimaendeleo.
Mgombea ubunge jimbo la Maswa mashariki , Daktari George Lugomela akizungumzaAmeahidi akichaguliwa kuwa Mbunge,pamoja na Daktari Samia Suluhu Hassani kuwa Rais na madiwani wa CCM tatizo la hupatikanaji wa maji safi na salama litakuwa historia.
Amesema Serikali hipo katika mchakato wa awamu ya kwanza kuvuta maji kutoka ziwa victoria hadi wilaya ya Maswa ikiwemo jimbo la Maswa mashariki.
Akizungumzia miundombinu ya barabara Daktari Lugomela ameeleza Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Meatu hadi Maswa.
Akizungumza katika kampeni hizo,Mgeni Rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama mkoa wa Simiyu Shamsa Mohamedi amesema Serikali ya Rais Samia imefanya kazi kubwa kwa miradi ya maendeleo kila mkoa,wilaya,kata na vijiji.
Mwenyekiti wa Chama mkoa wa Simiyu Shamsa Mohamed akizungumzaAmeeleza yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya sita kila mtu anajionea mwenyewe na wala siyo kusimuliwa bali mwenye macho aambiwi tazama.
Mgombea Udiwani kata ya Nyalikungu Paul Jinunu amesema iwapo akichaguliwa changamoto za wananchi zitakwenda kuisha akishirikiana na Rais na Mbunge.
Kushoto ni mgombea udiwani kata ya Nyalikungu, Paul Jinunu, kulia ni Mwenyekiti wa Chama mkoa wa Simiyu Shamsa Mohamed wakiomba kura wananchi.



Post a Comment