DKT. CHOKOU TINDWA : UONGOZI WA SAMIA TANZANIA IMEPATA MAENDELEO MAKUBWA
Na Gustaphu Haule, Pwani
MJUMBE wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Dkt.Chakou Tindwa amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la ujenzi wa miundombinu ya barabara, umeme, elimu na afya kutokana na aina ya uongozi uliokuwa madarakani ndani ya miaka minne iliyopita.
Dkt.Tindwa amesema yeye ni mzoefu wa kutembea nchi nyingi duniani ikiwemo nchi jirani za Afrika lakini hali ilivyo katika nchi hizo katika sekta ya miundombinu ya barabara na hata umeme haziwezi kushindana na Tanzania kwa maendeleo yaliyofikia.
Tindwa , amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM katika Jimbo la Kisarawe uliofanyika Oktoba 26 /2025 katika Kitongoji cha Makurunge Kisarawe Mkoani Pwani.
Amesema mtandao wa umeme, miundombinu ya barabara pamoja na sekta nyingine Tanzania ipo juu na hiyo imetokana na utendaji bora wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwemo Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Tindwa amesema watu waache kusikiliza porojo za mitandaoni kwakuwa ndani ya miaka mitano CCM kimefanyakazi kubwa ya kuwaletea Wananchi maendeleo hususani katika sekta ya elimu, afya, umeme, barabara na hata maji.
Mjumbe wa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya Mkoa wa Pwani Dkt .Chakou Tindwa ( mwenye kofia katikati).Amesema kutokana na mafanikio hayo Wananchi wa Kata ya Kiluvya ,Jimbo la Kisarawe,Mkoa na Taifa ni vyema kujitokeza Oktoba 29 kuchagua viongozi wanaotokana na CCM akiwemo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt .Selemani Jafo na diwani.
"Niwaombe Wananchi wa Jimbo la Kisarawe ikifika Oktoba 29/2025 wote kwa pamoja twendeni tukamchague Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wake Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi ili waweze kuisimamia ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo,"amesema Dkt.Tindwa.
Amesema Mkoa wa Pwani miaka yote CCM imekuwa ikishika tano bora na anataka mwaka huu lazima mkoa ushinde na huwe katika tano bora ambapo aliwaambia Wananchi kuwa siku ya uchaguzi watoke kwa pamoja na majirani zao kwenda kumpigia kura Rais Samia pamoja na Dkt .Jafo .
Wana chama cha Mapinduzi ( CCM) Jimbo la Kisarawe katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kitongoji cha Makurunge Kata ya Kiluvya.Katibu wa Kamati ya ushindi Kanda ya Mashariki Hawa Ghasia amesema lengo lake kubwa katika mkutano huo ni kumuombea kura mama Samia kwakuwa kati ya watu ambao anagombea nao hakuna mwenye sifa ya kumzidi mgombea wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ghasia amesema kuwa Dkt .Samia amefanyakazi kubwa ya kuleta maendeleo hususani kusambaza umeme, kujenga madarasa na kujenga miundombinu ya barabara na mwaka huu kuna ilani ya Taifa ya mwaka 2025/2030 ambapo kwa upande wa Kisarawe itajenga Zahanati 17 na Kiluvya itapata kituo cha afya na itajengewa Shule za Sekondari tatu na moja itajengewa Kiluvya.
Hata hivyo , mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt.Selemani Jafo alitumia nafasi hiyo kusisitiza suala amani huku akisema amani ni kitu pekee kinachotakiwa kulindwa kwani bila amani hakuna maendeleo.





Post a Comment