HEADER AD

HEADER AD

RAIS WA CHAMA CHA WALIMU AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI CWT BUSEGA


>> DC Busega atia neno

Na Abdallah Nsabi,  Simiyu

RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Dkt. Suleimani Ikomba ameongoza waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Busega mkoani Simiyu Mwl. Kaswalala Elisha.

Akitoa salam za rambirambi rais wa chama hicho amesema marehemu Kaswalala atakumbukwa kwa misimamo yake ya namna alivyokuwa akiwapigania walimu kupata haki zao na alipenda walimu wapete haki zao wanazostahili.

      Rais wa chama cha walimu Tanzania Suleimani Ikomba akitoa salam za Rambirambi.

Amesema Kaswalala alikuwa siyo mwoga katika kupigania haki za walimu na akutaka waonewe.

Mkuu wa wilaya ya Busega Faiza Salim amesema atamkumbuka mwalimu kaswalala kwa misimamo yake na pia alikuwa ni mchapakazi na mpenda haki.


     Mkuu wa wilaya ya Busega Faiza Salimu akitoa salam za rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Busega.

Amesema Kaswalala enzi ya uhai wake hakupenda mtu aonewe mbele ya macho yake bali alipenda kuona haki inatendeka  na alimfahamu kupitia misimamo yake ya kupigania haki.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha walimu Mkoa wa Simiyu,Mathias Sinzika akimwelezea marehemu Kaswalala amesema Kaswalala alikuwa ni mkweli na mwadilifu katika kutekeleza majukumu yake ya kazi.

Kaswalala aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Busega alifariki Dunia Octoba 22,2025 katika mji wa Lamadi na amezikwa Octoba 25,2025 nyumbani kwao kijiji cha Mwabasabi wilayani Busega.

     Mwenyekiti wa Chama cha walimu mkoa wa Simiyu Mathias Sinzika akitoa salam za Rambirambi.

        Wenyeviti wa wilaya wa chama cha walimu Cwt za mkoa wa Simiyu wakitoa salam.


Jeneza la mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Busega mwl Kaswalala Elisha.


No comments