ENG KUNDO AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA JIMBO LA BARIADI
Na Abdallah Nsabi, Simiyu
WAKAZI wa jimbo la Bariadi Mjini, Mkoani Simiyu wameakikishiwa kuondolewa Changamoto zinazowakabili ikiwemo miundombinu ya barabara na ukosefu wa maji safi na salama.
Hayo yameelezwa na mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi( CCM) jimbo la Bariadi mjini Mhandis Andrea Kundo wakati akihutubia mikutano ya kampeni kata za mhango na Somanda.
Ameeleza kwamba, changamoto za jimbo la Bariadi zinafahamika na tayari zingine alizishughulikia wakati alipokuwa mbunge.
Amesema Serikali imekwishaanza mchakato wa kuvuta maji kutoka ziwa victoria hadi wilaya za Bariadi na Itilima huku akiwatoa hofu na kuwataka kuwa na subira kwakuwa siku si nyingi changamoto ya uhaba wa maji itakuwa ni historia .
Akizungumzia miundombinu ya barabara amesema tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa km 50 za kufungua barabara zote za kata.
Huku akiwahakikishia wananchi changamoto ya miundombinu ya barabara korofi inakwenda kutatuliwa na serikali na zote zitapitika kwa muda wote.
Mhandis Andrea Kundo ameeleza kuwa barabara nyingi ni korofi hasa nyakati za mvua za masika huku akiwaomba wamchague kuwa mbunge wa jimbo la Bariadi Mjini,pamoja na mgombea Urais Daktari Samia Suluhu Hassani na wagombea udiwani ili wakashughulikie changamoto na kuzitatua.






Post a Comment