HEADER AD

HEADER AD

HAMOUD JUMAA NA GODFREY MWAFULILWA WAWAOMBA KURA WANANCHI

Na Gustaphu Haule, Pwani 

MGOMBEA wa ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa na mgombea udiwani Kata ya Mtambani Godfrey Mwafulilwa wamewaomba wananchi kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 29,2025.

Pia wamewaomba wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupiga kura ili kuhakikisha Dkt .Samia Suluhu Hassan anapata kura nyingi na za heshima.

     Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto) akimnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Mtambani Godfrey Mwafulilwa (Kulia) katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika Oktoba 13/2025 katika viwanja vya Dege la Jeshi vilivyopo Kata ya Mtambani.

Jumaa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Kata ya Mtambani alipokuwa akizinduzi kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo uliofanyika katika uwanja wa Dege la Jeshi Oktoba 13/2025.

"Nimekuja katika mkutano huu kuwaombeni kura, mpigieni kura Diwani , mimi na bila kumsahau mgombea urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Jumaa amewaomba wananchi wasifanye makosa siku ya Oktoba 29  huku akiwasisitiza Wananchi hao siku hiyo wahakikishe wanatoka nyumbani mwao wakiwa pamoja kwa ajili ya kwenda kumchagua Dkt. Samia kwakuwa bila kufanya  hivyo watakuwa wamefanya makosa makubwa .

     Mgombea wa ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto) na mgombea udiwani Kata ya Mtambani Godfrey Mwafulilwa (Kulia) wakiwa katika jukwaa siku ya uzinduzi wa kampeni za Kata ya Mtambani zilizofanyika Oktoba 13/2025.

Jumaa ameongeza kuwa wakimchagua kuwa mbunge wa Jimbo hilo yapo mambo mengi ya kimaendeleo yatafanyika ikiwemo kujenga Shule mpya ya Sekondari yenye thamani ya Sh. Milioni 700 na shule hiyo itajengwa katika Kata ya Mtambani.

Amesema  mpango wa ujenzi wa shule za Sekondari kila Kata ulianza tangu alipokuwa Rais Hayyat Benjamin Mkapa,akafuata Rais Jakaya Kikwete, Hayyat John Magufuli na sasa mpango huo unaendelezwa na Dkt .Samia Suluhu Hassan.

               Mgombea wa ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa watatu kutoka kushoto akiwa na mgombea udiwani wa pili kutoka kushoto pamoja na viongozi wa CCM Kibaha Vijijini akiwemo mwenyekiti Mkali Kanusu wa kwanza kulia

Amesema CCM inajiamini kwakuwa na Rais kama mama Samia na endapo watachaguliwa Oktoba 29 wamejipanga kubadilisha Mamlaka ya Mji mdogo wa Mlandizi kuwa Mji wa kisasa kwa kujenga stendi nzuri ya mabasi, eneo la Kisasa kisasa kwa ajili ya kufanyia biashara na ukarabati wa machinjio.

"Ndugu zangu wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini mimi ni kijana wenu,mtoto wenu, kaka yenu natambua changamoto za Jimbo la Kibaha Vijijini kwahiyo naombeni mniamini kwa kunipigia kura nyingi Oktoba 29 ili kuhakikisha Kibaha Vijijini inasongambele kwa maendeleo,"amesema Jumaa.

Mgombea udiwani wa Kata ya Mtambani Godfrey Mwafulilwa amesema amekuwa diwani wa vipindi viwili katika Kata hiyo .

Amesema wakimchagua kitakuwa kipindi chake cha tatu lakini jukumu kubwa ni kwenda kuisimamia ilani ili kuhakikisha yote yaliyomo kwenye ilani hiyo  yanakwenda kutekelezwa ndani ya miaka mitano .

     Mgombea udiwani Kata ya Mtambani katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini Godfrey Mwafulilwa .

Mwafulilwa amesema kuwa wananchi wanatambua namna ambavyo maendeleo yamefanyika katika Kata ya Pangani .

Amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo mambo mengi ya kimaendeleo yatafanyika kwa kuunganisha nguvu za  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,mbunge  Hamoud Jumaa na diwani wao ambapo ameomba wananchi wakipigie kura Chama cha Mapinduzi.

          WanaCCM katika uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya Mtambani katika Halmashauri ya Kibaha Vijijini uliofanyika Oktoba 13/2025

No comments