HEADER AD

HEADER AD

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI AWAOMBA WANANCHI KUMPIGIA KURA


Na Alodia  Dominick, Bukoba

MGOMBEA ubunge (CCM) jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Jonstone Mutasingwa amewaomba wana jimbo hilo kumpigia kura na kuahidi kuwa, endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atakuwa nao bega kwa bega siku zote za shida na raha.

Mhandisi Jonstone ameyasema hayo leo wakati akifunga kampeini na kuwaomba wanajimbo la Bukoba mjini kumpigia kura siku ya kesho Oktoba 29, mwaka huu.

     Wananchi Bukoba mjini wakiwa katika mkutano wa kufunga kampeni

"Nawaomba wananchi wa jimbo la Bukoba mjini mpige kura kwa wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  kuanzia nafasi ya  Urais, mimi Ubunge na madiwani wote nawaahidi kuwa, mkicheka nitacheka na nyie mkilia nitalia na nyie kipindi chote cha Ubunge wangu." amesema Mhandisi Mutasingwa

Amewaomba makundi yote wakiwemo Machinga, Mama ntilie,  wafanyabiashara wakubwa na wadogo, Watumishi wa taasisi za umma na binafsi kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kupiga kura.

Mhandisi Mutasingwa ametumia nafasi hiyo wakati wa kufunga kampeini kwa kutambulisha wazazi wake baba na mama, ndugu zake pamoja na familia yake mke na watoto ambao wamepata nafasi ya kumwombea kura.

Meneja Kampeni wa Mhadisi Mutasingwa Amani Kajuna amesema imefanyika mikutano ya madiwani katika jimbo hilo zaidi ya 99 na  mikutano ya Mbunge zaidi ya 30 wakinadi wagombea  na sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Meneja kampeini wa Mhadisi Mutasingwa Aman Kajuna akiomba kura kwa wananchi Bukoba mjini.

"Tumekutana na nyinyi katika mikutano huko, tumeongea mengi,  tumeona vingi lakini zaidi tumeshuhudia miradi iliyotekelezwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi  (CCM)"

"Miaka mitano iliyopita tulikuwa tunawaeleza wakati mwingine ilikuwa ni ngumu kuelewa, lakini leo hii tunaongea tukiwa na vitu vinavyoonekana katika Manispaa yetu ya Bukoba hongereni sana kwa kuichagua CCM na ninawaomba kesho muichague CCM" amesema Kajuna.

Amesema kuwa, katika Manispaa ya Bukoba miradi yenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni 35.4 imetekelezwa katika serikali ya awamu ya sita ya Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema miradi hiyo iliyotekelezwa ipo miradi ambayo imemalizika na ipo miradi inayoendelea kutekelezwa kama barabara ya njia nne, soko kuu, kingo za mto Kanoni na stend kuu na kuwa, atafurahi upigaji kura ukitangazwa Dk Samia Suluhu Hassan akashinda kwa asilimia 100.

Amewaomba wananchi wa jimbo la Bukoba mjini kupiga kura za kishindo kwa Dk.  Samia, Mhandisi Mutasingwa na madiwani wote wa jimbo hilo.




No comments