MGOMBEA UDIWANI KATA YA NSHAMBYA ATAJA VIPAUMBE ATAKAVYOANZA NAVYO AKIPATA UDIWANI

Na Alodia Dominick, Bukoba
MGOMBEA udiwani CCM kata ya Nshambya Godson Gybson ambaye ni Mstahiki Meya mstaafu manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ametaja vipaumbele vitano atakavyoanza navyo atakapopewa ridhaa na wananchi.
Mgombea huyo ametaja vipaumbele hivyo wakati wa uzinduzi wa kampeini za uchaguzi katika kata yake uzinduzi uliofanywa na mgeni rasmi Mwenyekiti (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Burhan.
Mjumbe wa mkutano mkuu wilaya kutoka kata Nshambya akimwombea kula mgombea udiwani kata hiyo Godson Gybson.
"Kwa mwaka 2020 hadi 2025 kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tumetekeleza miradi ipatayo 55 na nimeishapita nyumba kwa nyumba kuinadi kwa wananchi wangu na kwa kipindi kijacho mwaka 2025 hadi 2030 iwapo mtanipa ridhaa tena ya kuwa diwani wa kata hii, miradi ya maendeleo ipatayo 21 itatekelezwa ambapo nitaanza na miradi mitano"
"Ili niweze kufanya haya lazima niwe na mafiga matatu, namuombea kura Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge Mhandisi Jonston Mutasingwa na mimi mwenyewe diwani Gibson Gypson" ameeleza
Naye mgeni rasmi Mwenyekiti (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Burhan amesema zaidi ya Tsh. Bilioni 9.3 zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleao kata ya Nshambya manispaa ya Bukoba.
Mwenyekiti Uvccm mkoa wa Kagera Faris Burhan akizumgumza na wananchi wa kata ya Nshambya katika mkutano wa kampeini wa mgombea udiwani kata hiyo.
Akimnadi mgombea huyo amewaomba wananchi kuwapigia kura wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge pamoja na Udiwani ili waendelee kuwaletea maendeleo.
"Miradi iliyotekekezwa katika kipindi kilichopita ni ya thamani zaidi ya sh. Bilioni 9.3 na miradi hiyo ni ujenzi wa barabara, elimu bila malipo, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa daraja la Kyebitembe linalounganisha kata ya Nshambya na kata ya Rwamishenye" amesema Burhan.
Ameeleza kuwa, wakati likitengenezwa daraja la Kyebitembe watu walibeza sana kuwa halitakamilika lakini baada ya kufunguliwa barabara ya njia nne watu wanaoishi kata za Kahororo, Kashai, Nshambya wanapita katika barabara inayopitia katika daraja hilo kwenda kata jirani za Hamugembe na Rwamishenyi.
Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu wilaya kutoka kata ya Nshambya Agnes Kagenda ametumia mkutano huo kupiga magoti na kuwaombea kura viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Mbunge mstaafu jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato ambaye ni mkazi wa kata hiyo amesema wananchi wampe ridhaa Gypson ili aweze kuiendeleza na kumaliza kuitekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo na kutekeleza miradi mingine mipya.
Byabato amewaomba wananchi kuwachagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kujiletea maendeleo katika manispaa ya Bukoba.
Aidha mgombea udiwani viti maalumu(CCM) kata ya Nshambya Jasintha Kakokoo amewaomba wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu kwa ajili ya kupiga kura za mafiga matatu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wa kwanza kulia ni mgombea udiwani kata Nshambya Godson Gybson katikati ni mke wake akimwombea kura na wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Kagera Faris Burhan akimnadi mgombea kwa wananchi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano
.jpg)
.jpg)


Post a Comment