HEADER AD

HEADER AD

MWILI WA MAREHEMU ASKOFU NOVATUS WAZIKWA

Na Alodia Dominick, Bukoba

MWILI wa marehemu Askofu Mkuu, Balozi Novatus Rugambwa ambaye alifariki dunia Vatican umepumzishwa rasmi katika kanisa kuu jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera.

Mwili huo umepumzishwa leo Septemba 29, 2025 katika kanisa kuu jimbo Katoliki la Bukoba baada ya Askofu Rugambwa kufariki Septemba 16 mwaka huu nchini Italia makao makuu ya kanisa Katoliki Vatcan.

Akiongoza misa kabla ya ibada ya mazishi Askofu mkuu wa jimbo kuu Katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa ambaye amewasihi waumini katika jimbo hilo kuendelea kumwombea pumziko jema.

   Mazishi ya Askofu mkuu, Balozi Novatus Rugambwa yaliyofanyika kanisa kuu Katoliki jimbo la Bukoba.

"Askofu Rugambwa alikuwa mtu aliyewatendea mema watu binafsi na jumuiya, alikuwa mtu mwema, myenyekevu, mwenye fadhira na mwenye upendo" amesema Kardinal Rugambwa

Amesema kifo cha Askofu Rugambwa aliyefariki akiwa na miaka 67 kiwakumbushe wakristo kuwa, hapa duniani wanapita na wanatembea na kifo hivyo wanapaswa kujiweka tayali kama wale wanawali watano  katika kitabu cha Mathayo ambao walikuwa wamejiandaa.

"Tuwe tayali kujiandaa na harusi na kuwa tayali kwa kukutana na Bwana wetu katika utukufu, tukiwa tumezijaza mafuta taa zetu yaani kwa kuimarisha imani yetu na kuwa na matendo mema ya kumpendeza Mungu ili siku itakapofika tuipokee kwa furaha" amesema Mwadhamu Cardinali Rugambwa

Naye Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania (TEC)  Askofu Wolfgang Pisa amesema kuwa, Askofu Rugambwa ni kati ya watu wachache waliovuka mipaka ya lugha, nchi pamoja na Mabara hapa duniani.


Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu mkuu Angelo Accatino ameeleza kuwa, Askofu Rugambwa alitimiza majukumu yake na alijaliwa vipaji vingi vya kibinadamu na vingine alivirithi kutoka katika familia aliyozaliwa hivyo Tanzania inapaswa kujivunia kumpata yeye.

Ikumbukwe kuwa, Askofu Mkuu, Balozi Novatus Rugambwa alizaliwa mwaka 1957 katika familia ya Benedicto Rwechungura Parokia ya Maruku wilaya ya Bukoba, mwaka 1986 alipata daraja la upadre na kuhudumu jimbo la Bukoba, mwaka 1987 alijiunga na chuo cha kipapa ambapo alijifunza sheria za kanisa na mambo ya kidpromasia.

Aidha, mwaka 2010 aliteuliwa na Papa 16 kuwa Askofu mkuu wa Tanzania na kuwekewa wakifu,  mwaka 2023 alianza kuugua na madaktari waligundua alikuwa na ugonjwa wa kiharusi na Septemba 16, mwaka huu alifariki dunia.

Ibada ya mazishi imeongozwa na Askofu mstaafu wa jimbo Katoliki la Sumbawanga Mhashamu Damian Kyaruzi.





No comments