HEADER AD

HEADER AD

POLENI NDUGU ZANGU

RIZIKI zitafuteni, atoaye ni Rabuka,

Hilo lizingatieni, acheni kutaabika,

zinatosha zenu fani, ya nini kuhangaika,

Mtoaji ni Rabuka popote takupatia.


Lengo lenu la kusoma, ni kupata kazi nzuri,

Itayowapa heshima, na mshahara Mzuri,

Na nyie mle na nyama, watoto wale vizuri,

Aitoaye riziki ni Rabuka si mwingine.


Msiishi kwa mashaka, Kwani mmekosa nini,

Kwa nini mnateseka, wakati mnazo fani,

Msije mkaumbuka, Kwa kujiweka rehani,

Maisha popote pale Tanzania ya Amani.


Shida mnazopitia, hakika ni mtihani,

Hofu zimewazidia, Kila Kona ni madeni,

Haya mimi nayajua, napenda kuwajuzeni,

Huruma nawaonea hizi shida hadi lini.?


Sauti yenu pazeni, haki yenu kuisaka,

Maisha yenu thamini, msiishi kwa mashaka,

Na kikao itisheni, mtashinda kwa hakika,

Heri ninawatakia na Mola awainue.


Huruma nawaonea, ndugu zanguni jamani, 

Haya nikiyasikia, ninaumia moyoni,

Ninapenda kusikia, mmejaa mifukoni,

Pole napenda kuwapa subira yahitajika.


Mengi nimeelezea, kwa huzuni na hisia,

Shairi ninalitoa, pole ninawapatia,

Mwishoni nimefikia, kitini ninarejea,

Heri ninawatakia katika maisha yenu.


Mtunzi

Sirdody

kilimanjaro Tanzania

0762396923 au

0675654955.

soyakijijini@gmail.com

No comments