WANAFUNZI MAHAHA SEC. WAHIMIZWA KUTOJIINGIZA KWENYE MAANDAMANO , VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

Na Abdallah Nsabi , Simiyu
MKURUGENZI wa Kiwanda cha kutengeneza mabomba cha MOLI OIL MILLS CO LTD , Milembe Emanuel amewaomba wanafunzi mkoani Simiyu kutokubali kushawishiwa kuandamana ama kufanya vurugu zitakazohatarisha amani wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba, 29, 2025.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne ,shule ya sekondari Mahaha iliyopo wilaya ya Baridi,mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabomba cha MOLI OIL MILLS CO LTD , Milembe Emanuel, akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne, shule ya sekondari Mahaha iliyopo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Pia amewahimiza wanafunzi kutotumia mitandao vibaya na badala yake waitumie kwa manufaa mazuri ya kuijenga nchi kimaendeleo.
" Niwaombe wanafunzi kuachana na habari za mitandaoni zinazowashawishi watu kuandamana wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 29 , na msijemkajitokeza kufanya vurugu.
" Vurugu zinahatarisha amani ya nchi , lakini pia tusitumie mitandao vibaya na badala yake tuitumie kwa nia njema inayojenga kwa maendeleo ya nchi yetu" amesema Mkurugenzi Milembe.
Milembe ametoa motisha ya zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma makundi mbalimbali ikiwemo kuchangia fedha kwa ajili ya maendeleo ya shule na vifaa vya kufundishia.
Jumla ya wanafunzi 124 wanategemewa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha nne shule ya sekondari Mahaha.
Wakati huo huo , Milembe amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutekeleza miradi ya maendeleo shuleni hapo kujenga vyumba vya nadarasa, maabara, na mabweni ya wanafunzi.



Post a Comment